ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 23, 2017

NAPE: SINA KINYONGO NA UAMUZI WA RAIS MAGUFULI


Aliyekuwa Waziri wa Habari,  Nape Nnauye amezungumza na Waandishi wa habari akiwa juu ya gari lake leo maeneo ya St. Peter Osterbay Dar es salaam  ikiwa ni saa chache mara baada ya taarifa kutoka Ikulu kutangaza kwamba uteuzi wake umetenguliwa.

Hali hiyo imetokana na Jeshi la Polisi kuuzuia mkutano huo ambapo RPC Kinondoni alifunga barabara kwa gari kuzuia Gari ya Nape huku akiwataka waandishi wa habari watawanyike mara moja.

Haya ni machache ambayo Nape kayaongea

1.Nia ya mkutano wangu haikuwa mbaya. Nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari lakini Polisi wanakuja kunizuia.

2.Mnajua ni kiasi gani nimepigana kuirudisha CCM madarakani? Miezi 28 nimelala porini leo mtu anakuja kunitolea bastola.


3.Jana nilisema kuwa kuna gharama za kulipa wakati unatetea haki za watu. Na nilisema kuwa nipo tayari kuilipa gharama hiyo.

4.Sina kinyongo na serikali wala chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa.

5.Niliikuta CCM iko shimoni nikaitoa huko. Uzalendo wangu ndani wa CCM si wa kutiliwa shaka.

6.Kina Kawawa walikuwepo wakapita, sisi tutapita, lakini tujiulize tutawaachia watoto wetu Tanzania ya namna gani?

7.Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe.

8.Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali.

9.Nilitamani sana kuendelea kufanya kazi na ninyi waandishi wa habari lakini muda wa aliyeniweka umefika akaamua niondoke.

10.Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza

11.Vijana naomba msimamie haki yenu

4 comments:

Unknown said...

Duu mbona ghafra huo uteuzi wa Waziri wa habari,utamaduni na michezo?.Nape ni mzoefu sana na utawala uliopo madarakani,Nitashangaa sana akiona jambo la kutenguliwa uwaziri ni jambo geni,Mungu ametujaria kiongozi mchapakazi asiyeangalia sura wala cheo cha mtu,pale anapoona mambo hayaendi vile yanavyotakiwa hacheleweshi.Sasa basi Nape anatakiwa ajue polisi si kwaajiri ya kuzuia mikutano ya vyama pinzani tu,polisi haina mwenyewe ni yakila mwananchi.Sasa tulia umsikilize Rais atakupa kazi gani nyingine ya kufanya.Tunakushukuru kwa jinsi ulivyofanya kazi na waandishi wa habari Tanzania.

Anonymous said...

Kosa la Nape
ni nini? na makonda ni nani Tanzania mpaka Rais anaingilia kazi za mawaziri
Aliowateua. Nape kama sikosei aliongea vizuri kuhusu kamati aliyoiunda
Atajutia kumkashifu Lowassa wakati wa kampaini.Ukiangalia utawala wa Idd Amini utaweza kujua Tanzania ya kesho.

Anonymous said...

Makonda ni nani serikalini? Makonda ni mkuu wa mkoa wa Daresalam. Na ni daresalam kwenye kitovu cha uhalifu Tanzania. Na ni dar kwenye bandari kuu Tanzania. Na daresalam kwenye uwanja mkuu wa ndege wa Tanzania. Na ni daresalam yenye idadi kubwa ya watu Tanzania kuliko mkoa mwengine wowote ule Tanzania. Na ni daresalam kwenye maslahi makubwa ya watanzania na Tanzania kuliko sehemu nyengine yeyote ile Tanzania kwa hivyo kwa kifupi utaona makonda ni nani kimajukumu katika maendeleo ya Tanzania. Watu wengi wanasiasa hasa wabunge wakuchaguliwa na wananchi na mawaziri Tanzania kama vile wanabeza mkuu mkoa ni nani? Eti wanahoji kwanza kachaguliwa na raisi na sio na wananchi na kama vile wanabeza na kuona kuwa wao wanahaki zaidi ya kusikilizwa kuliko wakuu wa mikoa kitu ambacho ni kosa kubwa. Mkuu wa mkoa ni mteule wa Raisi na kupitia kura za wananchi zilizomchahua muheshimiwa raisi ndizo zilizomchagua mkuu wa mkoa kwa hivyo kiusahihi kabisa mkuu wa mkoa kachaguliwa na wananchi. Kum'beza na kumdharau mkuu wa mkoa ni kmdharau aliempa nafasi hiyo ambae ni raisi. Mkuu wa mkoa ni raisi wa mkoa na si mbunge au meya wanaoweza kuchukua nafasi yake na wote wanatakiwa kufanya kazi chini yake kwa kuwa yeye ni mwakilishi mkuu wa serikali. Kuhusu raisi kuingilia kazi za mawaziri ni sawa na kumuuliza boss wako kwanini unanielekeza jinsi ya kufanya kazi? Mwisho wa siku ni magufuli atakae kuja kujibu hali ya maendeleo ya nchi na sio Nape au ulishawahi kusikia katika siasa za Tanzania wakimtaja au kumtupia lawama waziri yeyote wakati wa serikali ya kikwete? Lawama na malalamiko yote ni kikwete tu licha ya kuwa watendaji wake kwa kiasi kikubwa ndio waliomuangusha.

Anonymous said...

Magufuli amemfukuza kazi Nape eti kwa sababu amemkosoa Msukuma mwenzake Makonda ambaye alishambulia kituo cha habari (Clouds FM). Huu ni ukabila usio na tija. Maendeleo gani hayo tunayoyataka na ambayo Magufuli anayaimba wakati hakuna uhuru wa habari (Dictatorship)? Hajui kumfukuza Nape ni kosa kubwa sana, kwani Nape ameisaidia sana CCM na Magufuli wakati wa mbio za uchaguzi kwa kumpigia debe na kumweka madarakani. Vile vile Nape anao wafuasi wengi sana vijana na anapendwa sana nyanda za juu kusini na mikoa ya kusini. Kama Nape ataamua kuingia kwenye mbio za Urais uchaguzi ujao kupitia chama chochote kile, basi politically "Bulldozer" atatoka jasho. Magufuli atakuwa Rais wa kwanza katika historia ya Tanzania kuwa madarakani kwa Awamu moja tuu, maana hatawezi kuwavutia wafuasi wengi kutoka mikoa ya kusini, ambayo ndiyo ngome kubwa ya CCM na ambao asilimia zaidi ya Themanini (80%) walimpigia kura Magufuli dhidi ya Lowasa.