ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 29, 2017

RAHA ZA PWANI ZATINGA KATIKA ANGA ZA MAREKANI

Katika jitihada za Kuikuza lugha tamu na Adhim ya Kiswahili, pamoja na Kuutangaza utamaduni wa Mswahili, mwenye asili ya Mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, hususan katika nchi za Afrika Mashariki na kanda za Maziwa makuu, kampuniu ya Swahili Media Network, ya hapa mjini Washington, DC, imezindua rasmi Tamasha litakalo fanyika kila mwezi, lijulikanalo kwa jina la RAHA ZA PWANI, kwa lengo la ku-Wahamasisha Wadau na Raia wa Marekani, juu ya utamaduni huu wa Mswahili.
Uzinduzi rasmi wa RAHA ZA PWANI ulifanyika siku ya Jumapili, tarehe 26 February, na kwamba tamamsha la mwezi huu wa March, lenye Mwito Mbiu,  "Mwanamke Kujipenda," litafanyika siku ya Ijumaa, tarehe 31 March, 2017, kwenye Ukumbi wa The Hampton Inn, Baltimore Avenue, MD 20740, kuanzia saa 10:00 za Jioni hadi saa 5:00 za Usiku. Rai wote wa DMV wanakaribishwa katika usiku huu wa Kuji-Tanafasi, na kuenzi mafanikio au Maendeleo ya Mwanamke Duniani.
Akizungumza na Wahariri wa Vijimambo Blog, Mkurugenzi wa Swahili Media Network, Bwana Steve Mgaza, alisema kuwa lengo la RAHA ZA PWANI, ni kuwapa fursa wananchi wa Marekani, wakutane ana kwa ana, na marafiki zao Waswahili, ili waweze kujifunza mengi, kwa kushiriki katika pamoja mijadala na midahalo ya Kiswahili, kusikiliza na kucheza Muziki wa Mwambao-hususan Taarab, pamoja na kuona vivutio vya Mavazi ya Pwani, na kupata Vionjo vya Mwambao.
Akiwa katika ziara fupi nchini Tanzania na Kenya, Bwana Mgaza alisema, kuwa wakati wake mwingi aliutumia kutembelea taasisi za Umma zinazo simamia Sanaa na Muziki, ili kuchangia mawazo ya jinsi ya kuutangaza utamaduni na Sanaa za Waswahili nchi Marekani na Duniani kote. Halikadhalika, alikutana na vikundi vya Wasanii mbali mbali na Wabunifu wa mitindo ya Mavazi, ambao wengi kwa jumla wanaunga mkono na kujipanga waweze kushiiriki katika Tamasha za RAHA ZA PWANI za siku za usoni.
Aidha, Bwana Mgaza alisema, kila mwezi, RAHA ZA PWANI itakuwa na Tukio ama Mgeni Rasmi, pamoja na kuwapa fursa Wasanii mbali mbali waje Marekani kushiriki na kuonyesha sanaa zao Mubashara na kuwapa burudani Wadau na raia wa hapa DMV na katika miji mikoa mingine ya Marekani. Kwa maelezo zaidi --Piga Simu kwa Swahili Media Network - Namba: 202-730-6116 AU Namba: 202-684-0002


BWANA MGAZA AKIONGEA NA KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA SANAA LA TAIFA - BW GODFREY MNGEREZA, ALIPOKUWA MJINI DAR-ES-SALAAM. 
BWANA MGAZA AKIMHOJI BI BONA LEON MASENGE, AFISA SANAA
"VIWANGO NA UBORA WA SANAA" --BASATA
BWANA MGAZA AKIMHOJI MSANII MAARUUFU WA MUZIKI WA TAARAB TANZANIA - BI MOSSY SULEIMAN
TANZANIA JIVUNIE SANAA GROUP - DAR ES SALAAM

No comments: