Sunday, March 12, 2017

SHYROSE AWASILISHA MUSWADA BINAFSI KUSAIDIA WENYE ULEMAVU

Muswada binafsi wenye lengo la kutungwa kwa sheria ya kuwalinda albino umewasilishwa kwenye kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda. Muswada huo umewasilishwa bungeni na Mheshimiwa Shyrose Bhanji, mbunge wa Tanzania. Katika muswada huo, Bhanji ameelekeza haki za msingi zinazopaswa kutolewa kwa walemavu hao kutoka Serikalini, Taasisi binafsi na kwenye jamii zetu. Muswada huo kama utapitishwa na Bunge na hatimaye kukubalika na Marais wa Afrika Mashariki, utatumika kwa nchi zote za Afrika Mashariki na utakuwa umesaidia watu wenye Ualbino. Mheshimiwa Shyrose Bhanji "Ninamshukuru Mungu kwa fursa hii, " anasema Bhanji huku akisema kwamba kwake yeye jana ilikuwa ni siku ya furaha kubwa kwani hatimaye aliweza kuwasilisha bungeni muswada huo binafsi ambao unaoitwa The EAC Protection Of People with Albinism Bill 2017.
Mwanamuziki mahiri nchini Chege Chigunda aliandika katika page yake ya Instagram ambapo alimpongeza mbunge huyo kwa namna anavyofikiri na kutetea walemavu aliandika: “Hongera sana Mbunge wetu wa Afrika Mashariki Mhe. ShyRose Bhanji @shyrosebhanji kwa kupigania haki za ndugu zetu wenye ualbino. Hakika umeacha alama kubwa ya uwakilishi wako Tanzania na Afrika Mashariki. Tunajivunia.”  
Kipande cha nakala ya muswada huo.

1 comment:

KAYU said...

Dhuluma, unyama na uonevu wanaofanyiwa ndugu zetu hawa, hadi sasa bado serikali zetu hazijakuwa na "MIKAKATI MIKALI " ya kukomesha. Wote huwa tunaisahau kadhia hii na kujishughulisha na mengine yasiyokuwa na umuhimu mkubwa.Hata vyombo vyetu vya habari husubiri hadi anapouliwa albino na kukatwa viungo huandika mistari michache na kadhia huishia hapo. TUNAUNGA MKONO KWA DHATI NA TUNAPONGEZA HATUA HII YA KUWASILISHWA MUSWADA. Hatuishii tu kupongeza bali tunawaomba viongozi wetu walipe kipa umbele tatizo hili.Wawe na uchungu kama wangefanyiwa ndugu zao na hapa ndipo wangeweza kulitafutia tiba tatizo hili.HAIWEZEKANI hadi leo wenzetu hawa wawe wanachinjwa na kuishi kwa woga kama wanyama.HILI HALIKUBALIKI.(KAYU --Athens Greece)