Advertisements

Thursday, April 6, 2017

DC ARUMERU AHOJIWA NA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Alexander Mnyeti akihojiwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baada ya kuitikia wito wa kamati hiyo, Bungeni mjini Dodoma leo, kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na Matamshi aliyoyatoa mapema mwaka huu Wilayani Arumeru Mkoani Arusha yaliyokuwa na madai ya kuidharau Bunge. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Mkuu wa Wilaya Arumeru Alexander Mnyeti ameitwa na Bunge kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kulidhalilisha Bunge. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema hayo leo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni. Amesema Mnyeti ameitwa leo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, kinga na madaraka ya Bunge

No comments: