ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 20, 2017

KIKOSI KAZI CHA KUNUSURU MTO RUAHA MKUU CHAANZA KAZI

Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kulinda ikolojia ya mto Ruaha Mkuu ambaye pia Mkurugenzi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akiongea na Watendaji wa Wilaya ya Mufindi (haapo pichani) katika Mkoa wa Iringa wakati wa mkutano kati ya Wajumbe wa Kikosi Kazi na Watendaji wa Wilaya hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wialaya ya Mufindi wakisikiliza maoni mbalimbalimbali ya Wajumbe wa kikosi kazi cha kuimarisha ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu kilchoteuliwa na Mkamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania (hawapo pichani) 
.Katibu Tawala wa Mkoa wa mbeya Bibi Mariam Mtunguja akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kikosi kazi hiko kilipotembelea Wilaya ya Mufindi.

Halimashauri ya Wilaya ya Mufindi imepewa mwezi mmoja kuhakikisha vyanzo vote vya maji vinaainishwa, kutambuliwa na kuhakikisha shughuli zote zinazosababisha kukauka kwa vyanzo hivi zinaachwa mara moja. Aidha Halmashauri imeangizwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kutenga maeneo ya mashamba ya kulima chakula na maeneo ya kupanda miti ili wananchi wawe na ardhi ya kujitosheleza na endelevu ya kilimo cha mazao ya chakula. Kwa sasa miti inapandwa kila sehemu na vijiji vingi sasa havina maeneo ya mashamba ya kilimo cha vyakula ya kutosha na hivyo kusababisha wananchi kuendelea kuvamia mabonde kwa ajili ya kilimo cha Vinyungu.

Maagizo haya yametolewa na Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Taifa cha kunusuru na kuweka mikakakti endelevu ya kulinda ikolojia ya mto Ruaha Mkuu, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi alipokua akiongea wakati wa mkutano wa Kikosi kazi pamoja na uongozi wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Aidha ameangiza mpango kazi wa utoaji wa elimu kwa wananchi katika hali endelevu kwa vijiji vyote 121 ambao utawaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya Mto Ruaha mkuu na vyanzo vote vya maji uwasillishwe katika sekretariat ya kikosi kazi ndani ya siku nne ili kujua ni jinsi gani wilaya itahahakikisha suala la elimu kwa umma linakuwa endelevu.

Wakichangia katika kikao hiko, Wajumbe mbalimbali wa kikosi kazi hiko wamesisitiza juu ya Watendaji wa Wilaya hiyo kuwa makini katika utendaji wao wa kazi na kuhakikisha kuwa wanasimamia sheria za ardhi na Mazingira ili kuwezesha ikolojia ya mto Ruaha mkuu inatunzwa vizuri. Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi Mariama Mtunguja, alisisistiza haja ya kila mtendaji kujituma na kuacha kutoa visingizio vya ukosefu wa fedha kwa kila kazi ambazo hazijafanyika hata zile ambazo ni wazi hazihitaji fedha yoyote. Alihoji kwa nini hata kazi ya kuweka mipaka ya vyanzo via maji vinavyojulikana kwa kupanda miti ya asili katika mipaka hiyo kunasubiri fedha ya serikali kuu.

Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William alishukuru kikosi kazi hiko kwa kufika katika Wilaya yake na ameahidi kusimamia na kuyafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na kikosi kazi hiki. Aidha Viongozi mbali mbali wakiwemo Madiwani na Wevyeviti wa Halmashauri wamekubaliana na maelelezo ya kikosi kazi kuhusu hatua kali kwa watakaokaidi maagizo ya serikali kuhusu kunusuru mto Ruaha mkuu ili kunusuru mazingira na kuwepo kwa uhakika wa maji kwa watumiaji wote.

Kikosi kazi hicho kimeundwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni jitahada za kuweza kuokoa ikolojia ya mto Ruaha mkuu ambao unazidi kuharibika siku hadi siku kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji kutokana na shughuli mbali mbali za ki binadamu katika vyanzo vya maji ya mto huu.

No comments: