Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha kumi cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
Serikali imesema itaendelea kulipa madeni ya walimu kadri inavyoyapokea na kujiridhisha kwamba madeni hayo ni halali.
Serikali imesema itaendelea kulipa madeni ya walimu kadri inavyoyapokea na kujiridhisha kwamba madeni hayo ni halali.
Waziri mkuu Mhe.Khasim Majaliwa amesema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo.
Amesema Serikali imeandaa utaratibu mzuri wa kulipa madeni hayo kila yanapohakikiwa na kuwataka walimu kuendelea kufanya kazi zao kwa
bidii.
Awali mbunge wa Kilolo Mhe.Venance Mwamoto alimuuliza Waziri mkuu sababu za baadhi ya madeni ya walimu kulipwa kwa kusuasua na Serikali na mengine kutokulipwa.
No comments:
Post a Comment