ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 3, 2017

BENKI YA NMB YAISAIDIA TIMU YA SINGIDA UNITED VIFAA VYA MICHEZO VYA SH.MILIONI 10

Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Richard Makungwa (kulia), akimkabidhi Katibu wa Timu ya Singida United, Abdurahman Sima,  mipira na vifaa vingine vya michezo vyenye thamani ya sh,milioni 10 Dar es Salaam leo kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayoanza Agosti mwaka huu.
Katibu wa Timu ya Singida United, Abdurahman Sima (kushoto), akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea vifaa hivyo.

Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Richard Makungwa (katikati), akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo. Kulia ni Mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuph Mwandani.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Hapa ni makabidhiano ya jezi.
Vifaa vilivyokabidhiwa vikioneshwa kwa wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Richard Makungwa (katikati), akisisitiza jambo baada ya kukabidhi msaada huo.


Na Dotto Mwaibale

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10 kwa timu ya Singida United kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayoendelea kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo,  Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Richard Makungwa alisema msaada huo umelenga kusaidia timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa kwa ligi hiyo.

"Tumetoa msaada huu kwa timu ya Singida United kwa kwa ajili ya maandalizi ya ligi hiyo na hii ni kawaida yetu kusaidia timu mbalimbali pale tunapopata nafasi" alisema Makungwa.

Makungwa alisema licha ya benki hiyo kufanya shughuli za kibenki pia imejikita kuinua michezo nchini kwa kutoa msaada wa vifaa vya michezo.

Alitaja vifaa walivyotoa msaada kwa timu hiyo ni viatu vya mpira wa miguu, jezi na mipira vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 10.

Katibu wa timu hiyo Abdurahman Sima alisema vifaa hivyo walivyopata vitatumika kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo.


"Tunaishukuru benki ya NMB kwa msaada huu tunaomba wadau wengine kuiga mfano wa benki hii " alisema Sima.

No comments: