ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 7, 2017

CHADEMA watuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya Wanafunzi 32

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema wametuma salamu za rambirambi kufuatia kutokea kwa ajali mbaya iliyotokea leo na kusababisha vifo vya watu 32.

Katika salamu zao cha CHADEMA wamesema wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwani taifa limepoteza watu muhimu ambao wangelitumikia taifa katika siku zijazo.

"Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali mbaya Iliyotokea Leo tarehe 6 Mei,2017 Mkoani Arusha, Wilaya ya Karatu na kusababisha vifo vya wanafunzi 33 (watoto wa kike 16 na watoto wa kiume 17) waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent ya Mkoani Arusha.....Hakika taifa limepoteza watoto wake na vijana wa Kesho ambao wangelitumikia taifa letu siku zijazo". Alisema Mrema.

Aidha, chama cha CHADEMA pia wametoa pole kwa familia ya wafiwa, uongozi wa shule ya Lucky Vicent pamoja na wananchi kwa ujumla.
 
"Kwa majonzi makubwa tunatoa salamu za pole kwa wazazi, wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent,  uongozi wa Shule hiyo pamoja na wananchi wote wa Tanzania kwa msiba huu mkubwa na wenye kutia simanzi na huzuni kubwa...CHADEMA tutakuwa pamoja na familia za Marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo , tunawataka wanachama na watanzania wote bila kujali imani zetu tuwakumbuke wafiwa katika Sala /Dua ili Mwenyezi Mungu awatie ujasiri wafiwa katika kipindi hiki kigumu". Alisema Mrema

Pamoja na hayo, CHADEMA wamelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha ajali hiyo mbaya ili matokeo ya uchunguzi huo yatumike katika kuzuia ajali nyingine  isije kutokea katika siku zijazo.

No comments: