Advertisements

Monday, May 15, 2017

MBUNGE WA CCM ATOA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SH. MILIONI 33 VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI SHINYANGA


Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametoa msaada wa vifaa tiba ikiwemo vitanda vya kisasa vya kujifungulia,vitanda vya wagonjwa na viti vya wagonjwa katika vituo vya afya na zahanati katika halmashauri ya Shinyanga vijijini na Kishapu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 33.



Mbunge huyo amekabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha afya Tinde,zahanati ya Solwa,zahanati ya Nyashimbi,kituo cha afya Samuye katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini na kwa upande wa Kishapu ni Kituo cha afya Nhobola,Mwang’haranga,Dulusi na Songwa.


Vifaa hivyo vinatokana na jitihada zilizofanywa na mbunge huyo Azza Hilal Hamad kufika katika ubalozi wa China nchini Tanzania kuomba asaidiwe vifaa tiba hivyo ili kukabiliana na vifo vya mama na mtoto mkoani Shinyanga.
Akizungumza leo Jumamosi May 13,2017 wakati wa kukabidhi vitanda vitatu vya kisasa vya kujifungulia,vitanda 9 vya wagonjwa na viti vitatu (wheel chairs) vyenye thamani ya shilingi milioni 9.7 katika kituo cha afya Tinde kilichopo Shinyanga vijijini,mheshimiwa Hamad alisema vitasaidia kupunguza adha ya upungufu wa vitanda katika kituo hicho kilichojengwa mwaka 1920.
“Kituo cha afya Tinde kinahudumia tarafa yote ya Itwangi na kata za jirani,kilikuwa na upungufu wa vitanda 28,leo nimeleta vitanda hivi kusaidia wananchi wapate huduma bora,naomba wananchi muwe mstari wa mbele kuunga mkono shughuli za maendeleo,ni aibu kuona kituo hiki kilichojengwa kabla ya uhuru kikiwa hakina majengo ya kutosha ikiwemo nyumba za watumishi na wodi kwa ajili ya wagonjwa”,alieleza Hamad.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akipokelewa kwa shangwe katika kituo cha afya Tinde kilichopo Shinyanga vijijini alipofika kukabidhi vitanda vya kisasa na viti vya wagonjwa vyenye thamani ya shilingi milioni 9.7
Wacheza ngoma ya Kiswezi "Waswezi" wakimpokea mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwahutubia wakazi wa kata ya Tinde wakati akikabidhi vifaa tiba hivyo 


Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad  (CCM) akizungumza katika kituo cha afya Tinde


Wananchi wakimsikiliza mheshimiwa Azza Hilal Hamad
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwasisitiza wananchi kuchangia shughuli za maendeleo ikiwemo kujitokeza kuchangia ujenzi wa majengo katika kituo cha afya Tinde ambacho kilijengwa mwaka 1920 lakini mpaka sasa hakina majengo ya kutosha
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliwataka watoa huduma katika kituo cha afya Tinde na wananchi kutunza vifaa tiba alivyokabidhi katika kituo hicho

Viti vya wagonjwa,vitanda vya kujifungulia kwa akina mama na vitanda vya kulalia wagonjwa vilivyotolewa na mbunge Azza Hilal kwa ufadhili wa ubalozi wa China nchini Tanzania

Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza na wananchi wa Tinde
Vitanda vikiwa eneo la tukio
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  akimkabidhi Mganga Mkuu wa kituo cha afya Tinde,Dkt. Dama s Mnyaga Nyansira,shuka kwa ajili ya vitanda vya kulalia wagonjwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akikabidhi vitanda vya kujifungulia akina mama,vitanda vya wagonjwa na viti vya wagonjwa
Mtoto akiwa amekaa katika kiti cha wagonjwa wakati mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akikabidhi vifaa tiba katika kituo cha Tinde
Wananchi wa Tinde wakimpa zawadi ya Kondoo,mbunge Azza Hilal Hamad baada ya kufurahishwa na zawadi ya vitanda na viti vya wagonjwa katika kituo cha afya Tinde
Furaha ikaendelea kuonekana-Mkazi wa Tinde akiwa amembeba mheshimiwa Azza Hilal Hamad
Wakazi wa Tinde wakifurahia na mbunge wao 


Diwani wa kata ya Tinde Japhary Kanolo akizungumza katika kituo cha fya Tinde


Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

Katibu wa Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Abdallah Kirobi akimshukuru mheshimiwa Mbunge Azza Hilal Hamad kuwakumbuka akina mama kwa kuwaletea vitanda vya kisasa vya kujifungulia
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini Secilia Ismail akizungumza katika kituo cha afya Tinde ambapo alisema Mbunge Azza Hilal Hamad ni mbunge anayetakiwa kuigwa katika jamii kwani anajua thamani ya maendeleo na anajali wananchi 
Watoa huduma katika kituo cha afya Tinde na wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Katibu wa Jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Masanja Salum akizungumza katika kituo cha afya Tinde
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Angel Robert akizungumza katika kituo cha afya Tinde
Mganga mkuu wa wilaya ya Shinyanga vijijini Dkt. Amos Mwenda akimshukuru mbunge Azza Hilal Hamad kwa kuwakumbuka akina mama wa wilaya ya Shinyanga kwa kuwaletea msaada wa vifaa tiba kwani zahanati na vituo vya afya vinakabiliwa na changamoto nyingi hivyo msaada huo utasaidia kupunguza adha wanazopata wa akina mama na wagonjwa
Wakazi wa Tinde wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Watumishi katika kituo cha afya Tinde wakisoma taarifa ya kituo hicho,Kulia ni Peter Zabron,mwingine ni Mary Joseph Burudani ikaendelea- Waswezi wakiimba na kucheza Mtaalam wa Mashairi Anthony Meja akisoma shairi kwa ajili ya Mheshimiwa Azza Hilal
Msanii wa nyimbo za asili Mama Ushauri akiimba wimbo wa kumpongeza mheshimiwa Azza Hilal Hamad kwa kutoa msaada wa vitanda kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati mkoa wa Shinyanga
Mbunge Azza Hilal Hamad akicheza na Mama Ushauri
Burudani inaendelea
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikumbatiana na Msanii Mama Ushauri
Wanenguaji wa msanii Mam Ushauri wakicheza kwa madoido
Vijana wa msanii Mama Ushauri wakionesha mbwembwe zao wakati wakitoa elimu ya Ugonjwa wa Ukimwi kwa njia ya vituko
Vijana wa msanii Mama Ushauri wakiendelea kuonesha mbwembwe zao.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments: