Advertisements

Thursday, May 11, 2017

MISS TANZANIA AKABIDHIWA GARI LAKE LEO

Mrembo wa Tanzania, Diana Edward amewataka warembo wanaoshiriki katika mashindano ya Miss Tanzania kuwa wavumilivu ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za mashindano hayo zinazotokana na matatizo ya kiuchumi.
Shindano la Miss Tanzania lilifanyika Oktoba 29 mwaka jana mjini Mwanza na kampuni ya Lino ilishindwa kukabidhi zawadi ya gari baada ya mdhamini wa kwanza aliyeahidi kutoa zawadi hiyo kujitoa hatua za mwisho baada ya shindano hilo kuhamia Mwanza.
Kutokana na hali hiyo, kampuni ya Lino ilihaha kila kona kutafuta mdhamini wengine na kuwapata uzalishaji na usambazaji wa vipodozi asilia, Grace Product Ltd na duka la kuuza vito ya Gift Jewellers ambapo kwa pamoja waliamua kununua gari aina ya Suzuki Swift yenye thamani ya Sh 9milioni liyosajiliwa kwa namba T625DKL.
“Mbali ya kuwa mvumilivu, mrembo unatakiwa kuwa na nidhamu, nilisubiri zawadi hii kwa muda mrefu, najua matatizo ambayo yalikuwepo na ndiyo maana nilivumilia mpaka hii leo (jana), nashukuru kwa kupata zawadi na sasa nitaendelea vizuri na shughuli zangu za kazi za jamii,” alisema Diana.
Alisema kuwa kwa kupitia gari hilo, atafanya kampeni yake ya kupiga vita mimba za utotoni na unyanyasaji kwa wanawake kupitia kampuni yake aliyoisajili.
“Naomba warembo wajitokeza kushiriki katika mashindano ya urembo, ni mashindano mazuri sana yenye kujenga mtu na kumpatia kipato, tokea nimalize mashindano, nimeweza kupata dili mbalimbali ambazo sikutaka kuziweka wazi kwenye jamii, zimekuwa ni shughuli zangu za kila siku,” alisema.
Mkuu wa Itifaki wa Kampuni ya Lino, Albert Makoye alisema kuwa wameishukuru wadhamini wao na kwa sasa wanaanza pilika pilika za mashindano ya mwaka huu.
“Ni faraja, tulipewa muda wan a serikali kuwa ifikapo Mei 30 mwaka huu tuwe tayari tumekamilisha zawadi za warembo, tumefanikisha kupata gari kutoka kwa Grace Products na Gift Jewellers, sasa tunaanza ukurasa mwingine,” alisema Makoye.
Mkurugenzi wa Grace Products ltd, Elizabeth Kilili alisema kuwa ameamua kudhamini zawadi ya gari kutokana na kuvutiwa na mashindano na hasa Diana ambaye anatumia vipodozi vya asili.
Mhasibu Mkuu wa duka la Gift Jewellers, Faudhia Salum alisema kuwa wamemua kuwezesha zawadi ya gari hiyo, kama moja ya shughuli zao za kijamii. Salum alisema kuwa wao kama wauzaji wa vito wamefarijika sana kusaidia mashindano hayo na hasa ukizingatia kuwa vito vingi uvaliwa na akina dada kwa lengo la kupendeza.

No comments: