ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 11, 2017

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA MGENI WAKE RAIS WA AFRIKA KUSINI,JACOB ZUMA LEO JIJINI DAR

 Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma pamoja na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu na wananchi waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017.
 Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma akimueleza jambo  mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11, 2017.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa sambamba na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma mapema leomara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017.
 Rais Dkt Magufuli akimsikiliza Makamua wa Rais,Samia Suluhu Hassan wakati wa mapokezi ya Rais wa Afrika Kusini,Jacob Zuma mapema leo kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar
 Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini,Jacob Zuma akisalimiana na Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassani mapema leo kwenye viwanja vya Ikulu,jijini Dar,kushoto ni Rais Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo mara baada ya kumpokea mgeni wake
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpigia makofi mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma alipokuwa akipiga ngoma,mara baada ya kuwasili na kupokelewa mapema leo katika viwanja vya Ikulu,jijini Dar Es Salaam .
  Muonekano wa njia ya kuingilia Ikulu leo tayari kwa mapokezi ya Rais wa Afrika Kusini,Mhe.Jacob Zuma
 Moja ya kikundi cha ngoma za asili kilichoshiriki kusherehesha mapokezi wa Rais wa Afrika Kusini,Mhe.Jacob Zuma katika viwanja vya Ikulu mapema leo jijini Dar.Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments: