ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 13, 2017

Acacia waikana ripoti ya pili ya makinikia

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, imezikataa taarifa zote zilizotolewa katika ripoti ya kamati ya pili iliyochunguza makontena 277 ya mchanga wa madini yaliyozuiwa.
Wameyasema hayo ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kupokea ripoti ya kamati ya pili ya wanasheria na wachumi waliochunguza sakata la mchanga wa madini.
Pia wametaka uchunguzi huru wa ripoti ya kamati ya kwanza na ya pili zilizoundwa na Rais Magufuli kuchunguza mchanga huo.
“Migodi yetu inafanya kazi kihalali, kwa kufuata sheria za Tanzania, hata usafirishwaji wa mchanga huo unafanywa kwa kufuata sheria na kupata kibali cha usafirishaji,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa zuio la kusafirishwa mchanga huo haliiathiri Acacia pekee bali maisha ya maelfu ya Watanzania zaidi ya 36,200.
“Kampuni hii imekuwa ikiwekeza katika elimu, miundombinu na miradi ya afya na hivi vyote vitaathirika wakati zuio hili likiendelea.” Imesema taarifa hiyo.

No comments: