Advertisements

Wednesday, June 14, 2017

AZAM YAZITESA SIMBA, YANGA

Mshambuliaji aliyejiunga na Azam kutoka Kagera Sugar, Mbaraka Yusuph
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) jana lilitangaza kufungua dirisha la usajili kwa klabu za Ligi Kuu Bara, ligi daraja la kwanza na la pili.

Taarifa ya TFF kwa vyombo vya habari jana ilisema dirisha la usajili litafunguliwa Juni 15 na kufungwa Agosti 6 mwaka huu.

Tayari timu zimeshaanza kufanya mazungumzo na wachezaji lakini kwa timu zilizomaliza nafasi ya nne bora msimu uliopita, Azam ndio imeonekana makini katika usajili wake kwani tayari imeshasaini mkataba na wachezaji watatu wa maana na kuwaacha Simba na Yanga wakicheza na vyombo vya habari.

Azam imeshasaini mkataba wa miaka miwili miwili na Mbaraka Yusuf kutoka Kagera Sugar, Salmin Hoza wa Mbao FC na Waziri Junior kutoka Toto Africans ya Mwanza. Wachezaji hao wote walikuwa wakiwaniwa na miamba ya soka nchini Simba na Yanga.

Tangu juzi Azam chini ya Meneja wake Mkuu, Abdul Mohammed imekuwa ikisambaza picha kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zikionesha wakisaini mikataba na wachezaji hao makinda.

Hata hivyo, uongozi wa Kagera jana ulipinga hatua ya Azam kuingia mkataba na Mbaraka wakisema bado mchezaji hao kwa vilealikuwa na mkataba nao wa miaka mitatu.

HABARI LEO

No comments: