ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 23, 2017

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA KILWA YAFANYA ZIARA KATIKA KISIWA CHA SONGO SONGO

Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Wapili kushoto) walipotembelea mitambo ya Gesi Songas iliyopo katika kisiwa hicho juzi. 
Ofisa Usalama wa Kampuni ya Pan African Energy inayochakata na kusafirisha Gesi kutoka Kisiwa cha Songo Songo, Baraka Melchiory (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (kushoto) kuhusu hali ya usalama na namna ya kujikinga na majanga pindi itokeapo itilafu katika mradi huo. Mkuu wa Wilaya aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya katika ziara yake kutembelea mradi wa Songas juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Kushoto) akizungumza na Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas katika kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy. Mkuu wa Wilaya ya Kilwa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya katika ziara yake juzi. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Zablon Bugingo akizungumza na Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas kutoka Kampuni ya Pan African Energy, Andrew Hooper wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama walipotembelea Kisiwa cha Songo Songo kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hizo kijijini hapo.
Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (katikati) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai namna mitambo ya kuchakata Gesi inavyofanya kazi wakati wa ziara yao walipotembelea chumba maalumu (Control room) katika mitambo ya Gesi Songas iliyopo katika kisiwa hicho juzi. 
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizungumza na Viongozi wa Kijiji cha Songo Songo baada ya kukagua ujenzi ya nyumba ya mwalimu kijini hapo na kubaini mapungufu kadhaa, mkuu wa wilaya huyo aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kutembelea kijijini hapo juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizindua Choo katika Shule ya Msingi iliyopo katika Kijiji cha Songo Songo kilichojengwa na Taasisi ya Fanjove, mkuu wa wilaya huyo aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kutembelea kijijini hapo juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizungumza na wanakijiji cha Songo Songo baada ya kukagua miradi mbalimbali ya kijiji hicho iliyojengwa na makampuni yanayo endesha shughuli mbalimbali kijijini hapo. Mkuu wa wilaya huyo aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kutembelea kijijini. (PICHA ZOTE NA VENANCE NESTORY)

No comments: