Afisa Mazingira wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Bi.Esther Masomhe, (kulia), akizungumza jambo wakati wa mazungumzo ya meza ya duara kuhusu mazingira kwenye Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Juni 5, 2017, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute iliyoandaa majadiliano hayo, Bw. Habib Miradji.
NA
KVIS BLOG/Khalfan Said
MANISPAA
ya Ilala jijini Dar es Salaam imesema iko kwenye mkakati mkubwa wa kutengeneza
bustani za kupumzika wananchi na tayari wameanza kuboresha maeneo hayo kwa
kuanzia na eneo bustani ya Samora (Kaburi la Sharif), barabara ya Samora.
Akizungumza
kwenye mdahalo wa mazingira uliotayarishwa na Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue
Institute ya jijini Dar es Salaam leo Juni 5, 2017, Afisa Mazingira wa Manispaa
hiyo, Bi.Esther Masomhe, alisema, pamoja na vipaumbele vingi ambavyo Manispaa
hiyo inakabiliwa navyo, lakini moja ya hatua inazochukua ni kupendezesha jiji,
(City beatification).
“Kuna
maeneo tayari tumeanza nayo kama vile bustani ya Samora pale kaburi la Shariff,
barabara ya Samora, bustani ya Mnazi Mmoja namba mbili eneo laMcahfukoge,
tunakusudia kuiboresha bustani hiyo ili wananchi wapate mahala pazuri pa
kupumzika.” Alisema Bi.Masomhe.
Akifafanua
zaidi alisema, Wilaya ya Ilala ndiyo kitovu cha jiji la Dar es Salaam hivyo
Manispaa inachukuajuhudi mbalimbali kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa katika
muonekano mzuri kwa kuboresha mazingira na bustani zake.
Aidha
Afisa huyo wa Mazingira wa wilaya ya Ilala alisema, kwa kuzingatia kauli mbiu
ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani, ““Hifadhi Mazingira, kama Muhimili wa
Maendeleo ya Viwanda”
“kauli
mbiu hii ina maana kuwa viwanda vingi hapa nchini vimejengwa bila kuzingatia
uhifadhi wa mazingira, utakuta mtu mwenye kiwanda, anashindwa kuhifadhi maji
taka anayozalisha na badala yake anatiririsha kwenye mito, ambako huko kuna
viumbe hai, sihilo tu lakini pia kuna watu wanaendesha kilimo cha mboga mboga,
kwa vile maji wanayotumia ni hayo hayo ya mto ambayo tayari yanakuwa
yamechanganyika na maji taka ya viwandani, walima bustani hutumia maji hayo
kunyweshea bustani zao na hivyo kuwalisha wananchi mboga mboga zenye kemikali, nah
ii ni hatari kwa afya,” alisema
Alisema
kwakuwa sheria zipo wazi, watasimamia sheriahizo kikamilifu ili kuhakkiikisha
kiwanda kitakachoanzishwa kwenye Manispaa knazingatia uhifadhi wa mazingira.
Naye
Mwenyekiti wa mdahalo huo, ambaye pia ni mdhamini wa taasisi hiyo ya
Kilimanjaro Dialogue Institute, Bw. Habib Miradji amesema, “hakuna mtu ambaye
hafahamu umuhimu wa mazingira, lakini kumekuwepo na tatizo kubwa la
kimazingira, sisi tunaetembea dunia tunaona kuna milima misitu ya asili na
mbuga, kwa kweli inabidi ukae ufikirie jinsi maliasili ilivyotunzwa, lakini hapa kwetu, vitu kama hivi havipo, ilikuwa zamani tu maana hata milio ya ndege na
miti asili imetoweka.” Alisema.
Bw.
Miradji alihoji nini mikakati ya Manispaa katika uhifadhi wa mazingira kwani
maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu hususan uswahilini, (urban slams) haya yanakuwa na ongezeko la watu kwa
haraka, familia moja inawezakuwa na watu 10 na zaidi, nini mkakati ya Manispaa
katika kukabiliana na misongamano ya watu?
Akijibu
hoja hiyo Bi. Masomhe alsiema, kumekuwepo na mikakati mbalimbali ikiwemo ya
utoaji elimu mashuleni, kupitia klabu za mazingira za shule, lakini pia
kuboresha miundombinu kwenye maeneo hayo na kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo
hayo kupitia kwa maafisa afya wa Manispaa ambao hutembelea mara kwa mara ili
kutoa elimu ya usafi wa mazingira.
Bi.Esther Masomhe, akizungumzia mikakati ya Manispaa yake kuhusu mazingira na utunzaji wake
Mwenyekiti wa mdahalo huo, ambaye pia ni mdhamini wa taasisi hiyo ya
Kilimanjaro Dialogue Institute, (KDI), Bw. Habib Miradji
Mshauri wa masuala ya vyombo vya habari, Bw. Felix Kaiza akisikiliza kwa makini mjadala huo.
Katibu
Mkuu wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute (KDI), Bw.Hassan Mzighani,
(kulia), akizungumza kwenye mdahalo huo ambapo alisema anasikitishwa na jinsi
Manispaa inavyoshindwa kudhibiti maji taka, yakiwemo yale yanayosababishwa na
mvua na kutolea mfano nchi kama Norway, ambayo hupata mvua muda mwingi lakini
sio rahisi kukuta barabara au makazi ya watu yakiwa yamezingirwa na maji.
No comments:
Post a Comment