Advertisements

Tuesday, June 13, 2017

MAJALIWA AWAVALISHA VYEO MAAFISA WA MAGEREZA KWA NIABA YA RAIS

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka maaafisa na makamanda wa Jeshi la Magereza nchini waendelee kusimamia haki na usawa wanapotimiza wajibu wao.

Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na maafisa na makamanda wa jeshi hilo katika hafla ya kuwavisha vyeo maafisa 29 iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Akifanya kazi hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewavisha vyeo maafisa watano kuwa Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) na maafisa 24 kuwa Kamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza (SACP). Maaafisa hao walipandishwa vyeo Mei 25, mwaka huu.

“Ninyi ni viongozi wakuu katika mikoa mnayotoka. Huko kuna makamanda walio chini yenu na jamii inayowazunguka. Endeleeni kuwahudumiana na kulitumikia Taifa hili kwa weledi mkubwa. Endeleeni kusimamia usawa na haki katika kazi zenu za kila siku,” amesema.

Majaliwa amesema hana shaka na utendaji kazi wa jeshi la Magereza kwani watumishi wake ni waadilifu. “Jeshi hili linayo nidhamu ya hali ya juu, mbali ya jukumu lenu la ulinzi, mnafanya kazi nidhamu, weledi na uadilifu mkubwa,” amesema.


Amesema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kila siku na kwamba inajitahidi kuzishughulikia hasa baada ya kukamilisha zoezi la kuondoa watumishi hewa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha Jeremiah Nkondo kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo Tusekile Mwaisabila kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo . (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo, Afwililwe Mwakijungu kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo . (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) Manaibu Kamishina wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa aktika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla fupi ya kuvalisha vyeo Maafisa magereza iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa magereza aliowavalisha Vyeo kwa Niaba ya Rais John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni, 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: