ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 27, 2017

MEYA MSTAAFU YUSUFU MWENDA AMEWATAKA VIONGOZI WENYE UWEZO KUWASAIDIA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

 Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akizungumza wakati wa  hafla ya Idd aliyoindaa  nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. na kusheherekea na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha  Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .
 Mratibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Imra James Gabon akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa hiyo Prosper Mosha akizungumza. 
 Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akiwakabidhi  watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha  Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .baadhi ya zawadi aliyowaandalia (kushoto) Mratibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Imra James Gabon.
 Mke wa Meya Mama Tausi Yusufu Mwenda (mwenye nguo ya bluu) akimkabidhi moja ya zawadi Bi.Nuhimu Iddi anayetoka katika kituo hicho.
 Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akiwakabidhi zawadi watoto. 
 Wageni waalikwa.
  Watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha  Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .
 Shampeni ikifunguliwa.
Wageni waalikwa wakipata shampeni.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akipata shampeni.
 Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akiwaongoza watoto kupata chakula.
  Watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha  Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni  wakisherekea siku ya Iddi nyumbani kwa Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda.
 Wageni waalikwa.
 Mc aliyeandaliwa kwaajili ya sherehe hiyo akisisitiza jambo.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda amewataka wananchi, taasisi  na viongozi mbalimbali wenye uwezo kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa lengo la kuwakwamua na hali ya kiuchumi iliyopo kwa sasa.
Mwenda ameyasema hayo Jijini Dar es salaam jana katika hafla ya Idd aliyoindaa nyumbani kwake na kusheherekea na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha  Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni.
Alisema pamoja na mambo mengine,kufanya hivyo ni kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika harakati zake za kimaendeleo anazozifanya.

Alisema viongozi wananchi pamoja na jamii kwa ujumla haina budi kuendana na dhamira aliyonayo Rais Magufuli ya Taifa kujikwamua kiuchumi hususani kipindi hiki anapofanya mambo mbalimbali ya kuliletea maendeleo.
"Huu ni watati wa kila mmoja wetu kujitafakar, watoto hawa si yule mzazi aliyewazaa, bali wa taifa zima, hivyo ni vyema kila mmoja wetu akaona umuhimu wa kuwalea watoto hawa kiakili na kimaadili" alisema Mwenda.
Aidha alisema viongozi waliopo madarakani kwa pamoja  wanapaswa kushirikiana pamoja kuhakikisha maendeleo ya nchi hii yanapatikana kwa kasi huku akisisitiza kuwa pasipo ushirikiano huo hakuna maendeleo hayo yanayoweza kupatikana.
Awali Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa hiyo Prosper Mosha aliwataka wananchi mbalimbali wa manispaa hiyo kujitokeza kusaidia malezi ya watoto walioko vituoni kufuatana na utaratibu uliowekwa na manispaa hiyo.
Alisema Manispaa hiyo imeweka utaratibu wa kila anayehitaji kulea mtoto anayeishi katika miongoni mwa vituo vya watoto yatima, kupewa mtoto anayemuhitaji kwa lengo la kumlea.
"kwa sasa utaratibu upo wazi, kila anayehitaji kupata mtoto wa kumlea anapaswa kuja ofisini ili apate maelezo, ila utaratibu upo wazi kabisa kikubwa ni uzingatiaji wa sheria tulizoziweka" alisema Mosha.

No comments: