Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akisaiadiana na wachimbaji madini katika mgodi wa nyakavangala ili kuokoa mwili wa marehemu Nyenza
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alipokuwa akiwasili katika mgodi wa nyakavangala uliopo Kata ya malengamakali
NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Mhe. Richard Kasesela ameungana na wananchi katika zoezi la kutoa mwili wa mchimbaji madini kwenye mgodi wa Nyakavangala wilayani humo.
Mchimbaji huyo mdogo aliyetambuliwa kwa jina la Vaspa Nyenza, ulipatikana majirayasaa 7;50 usiku kufuatia juhudin hizo zilizoongozwa na Mkuu huyo wa wilaya kuanzia majira ya saa mbili asubuhi Juni 14, 2017.
“Zoezi limekuwa gumu mno kama uonavyo hadi wakati huu bado wenzetu walioko ardhini kuendelea na zoezi la kuufikia mwili wa marehemu hawajafanikiwa kwani kila wanapokaribia kuufikia, miamba laini inaporomoka,” alisema Mhe. Kasesela wakati zoezi hilo likiendelea.
Mkuu huyo wa wilaya aliwatahadharisha wachimbaji hao kuchukua tahadhari wakati wa kufanya shughuli zao ili kuepuka ajali kama hiyo iliyomkuta mchimbaji huyo.
No comments:
Post a Comment