Advertisements

Friday, June 16, 2017

WATUMIAJI WA JUMIA TRAVEL KWENYE SIMU WAONGOZEKA KWA 33%


Na Jumia Travel

 JUMIA Travel kwa kushirikiana na Google wameachia matokeo ya utafiti kuhusu maendeleo ya programu za mtandaoni (Progressive Web App - PWA) kwa kulinganisha na matumizi ya programu za kawaida za Android na IOS.

Ripoti ya utafiti huo inaonyesha kwamba kufuatia uimarishwaji kwenye vipengele vyote vya PWA, kampuni imeweka wazi kwamba kumekuwa na ongezeko la watumiaji wapya kwa 33% ukilinganisha na tovuti ya simu iliyopita. Pia kitu kingine cha kuzingatia ni kwamba kutokana na maboresho mapya kwenye PWA yameonyesha idadi ya watumiaji imeizidi ile programu ya awali kwa zaidi ya mara 12 na inazidi kukua, wakati nusu ya idadi ya watumiaji waliokuwa wanatembelea mtandao na kuondoka imepungua.      

Timu ya Jumia imeitengeza upya tovuti yake ya kwenye simu za mkononi kwa kutumia teknolojia za PWA na matokeo ya utafiti huu yameonyesha mafanikio mapya yaliyojieonyesha hususani katika
nyanja za uhifadhiji wa nafasi, ukaachi wa chaji wa betr na matumizi ya data ya intaneti. Uunganishwaji wa mfumo wa PWA kwenye tovuti ya Jumia kwenye simu umechochea matokeo mazuri zaidi kwa watumiaji, kuongezeka kwa watumiaji na hasa, kupungua kwa kiwango cha wasiokuwa wakitumia mtandao.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Travel, Bw. Paul Midy amesema kuwa, “Tunafanya kazi kwenye soko lililotawaliwa kwa kiasi kikubwa na watumiaji wa simu, kwa hiyo tunalenga kuleta teknolojia ya kisasa kabisa inayolenga kutumika kwenye masoko yote hata maeneo ambayo kasi ya intaneti ina changamoto.”

Ameendelea kwa kusema kuwa lengo la kampuni ni kuiinua teknolojia na kuendelea kuwekeza kwenye rasilimali



zitakazowaletea matokeo mazuri watumiaji, “Afrika ni soko ambalo linatumia simu kwa kiasi kikubwa, ndiyo kwanza tunaanza, na tunaamini kwa kuwatengenezea mazingira mazuri na rafiki ya matumizi ya simu ni jitihada kubwa katika kuyatimiza mahitaji ya wateja wetu.”

Naye kwa upande wake Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania, Bi. Fatema Dharsee ameongozea kuwa, “Matokeo ya utafiti huu uliofanywa na Google kwa kushirikiana nasi ni ishara nzuri kwetu kuonyesha kwa namna gani tunavyokuwa hususani katika maboresho ya huduma zetu. Ukizingatia kwamba watumiaji wa simu za mkononi mpaka hivi sasa Tanzania wapo zaidi ya milioni 40, ambayo ni sawa na ueneaji wa asilimia 83. Matumizi hayo kwa kiasi kikubwa yamechochewa na ueneaji wa intaneti ambao umekua na kufikia asilimia 19.86 kwa mwaka 2016 kutokea asilimia 17.26 mwaka 2015 nchi nzima kwa mujibu wa ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).”
 
“Ripoti inasema kwamba mtandao wa Jumia Travel kwenye simu za mkononi umeongezeka kuwa na watumiaji kwa 33%, idadi ya watumiaji wanaoutembelea na kuondoka imepungua kwa 50%, idadi ya watumiaji imeongezeka mara 12 ukilinganisha na ya wale wa Android na IOS, inatumia kiwango cha data mara tano chini zaidi, kiwango cha data kinachotumika katika kufanya miamala ni mara mbili chini zaidi, wakati nafasi inayohitajika kuihifadhi kwenye simu imepungua kwa mara 25 chini zaidi na pia ni rahisi zaidi kufanya maboresho ya mara kwa mara. Hivyo basi, takwimu zote hizi ni dhahiri kwamba maboresho ya kurahisisha huduma zetu hayana kikomo na Google wamelidhihirisha hilo kupitia ripoti yao ya kitaalamu zaidi juu ya programu yetu,” alihitimisha Bi. Dharsee.    

Ripoti iliyotolewa na Kituo cha Kimataifa cha Data (IDC) inaonyesha kwamba Afrika kiwango cha uingizwaji wa simu za mkononi kimeongezeka kwa kasi kwenye kila robo ya mwaka, na soko linatarajiwa kuongezeka maradufu, na hivyo kuchangia thelethi moja ya simu zote zinazosafirishwa kufikia mwishoni mwa mwaka 2017. Hii itazidi kuimarisha zaidi idadi ya wateja wanaopendelea kufanya manunuzi kwa njia ya simu. Pia ni tahadhari zaidi kwa wadau wa sekta ya biashara mtandaoni kuendana na mpango mkakati wa kutumia simu zaidi katika kuendesha shughuli zao.

No comments: