Wachezaji wa Yanga wakimbeba kipa wao Deogratias Munisi, baada ya kuamalizika kwa mchezo wao wa mashindano ya Kombe la SportPesa Super Cup na kutinga hatua ya Nusu Fainali ya michuano hiyo kwa kuwaondisha Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penati 5-3 baada ya kumalizika dakika 90 kwa timu hizo bila kufungana.
Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akimtoka beki wa Tusker, Corins SHivachi, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa (kulia) akichuana kuwania mpira na beki wa Tusker, James Situma, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Chirwa akijaribu kukatiza katikati ya mabeki wa Tusker
Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akijipinda kupiga shuti katikati ya mabeki wa Tusker, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
TIMU ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam,leo imetinga hatua ya Nusu Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup, baada ya kuifungashia vilago Timu ya Tusker ya Kenya kwa kuibanjua kwa jumla ya penati 5-3 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mikwaju ya Penati baada ya kumshukuru Dakika 90 kwa sare Tasa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es salaam
Penati za Yanga zilifungwa na Nadir Haroub 'canavaro', Obrey Chirwa , said Mussa na maka mwakalukwa.
Kwa upande wa Tusker waliofunga ni Noah wafula na Brian osumba
Juma Maadhi akichuana na beki wa Tusker James Situma
Said Mussa, akipiga hesabu za kumtoka beki wa Tuske
Kipa wa Yanga wakibebwa juu kushangilia ushindi leo dhidi ya Tusker.
No comments:
Post a Comment