Rumadha Fundi:
Yoga Teacher
Jinsi gani mafunzo ya Yoga na “Meditation” kwa mara nyingine tena ikidhihirisha na kubaini umadhubuti wake katika kujenga utulivu wa mawazo, kupunguza hasira na ukatili katika jamii kupitia utafiti sahihi uliofanywa nchini Afrika ya Kusini kupitia magereza yake ya usalama wa hali ya juu”Maximum Security Prisons” na kuweza kuwamudu wahalifu wenye matendo ya ukatili na fujo za hali ya juu na kuwa wasamalia wema katika jela hizo. Link:
Kwa zaidi ya maelfu ya miaka iliyopita, wana Yoga au Yogis wamekuwa wakifanya tafakari au Meditation kwenye mapango na milima kama moja ya njia kujitenga au epuka na kelele za jamii na kutafuta amani ya mawazo.
Kadri muda uavyo pita ndipo jinsi wana Yoga hao walipogundua jinsi ya kuelekeza mawazo yao kiundani kupitia mafunzo hayo. Mwili wa mwanadam kupitia uti wa mgongo, una sehemu au vituo muhimu saba ziitwazo Chakras kwa lugha ya “Sanskrit”, au “Psychic Centers” ambazo ndio muhimili mkuu kupitia tafakari kimawazo na hadi kufikia katika ubongo na kuimarisha na kupanua viwango vya fikra zetu.
Hapo ndipo neon “Mantra” kwa Sanskrit au neno mwanana linalo rudiwa kuambatana na pumzi tunazo pumua na kuishawishi akili itulia kupitia nidhamu ya Mantra muda wote tunavyo tafakari au kufanya “Meditation”.
CHAKRAS:
- MULADHARA – Testes/ Ovaries
- SVADISTHANA-Adrenal
- MANIPURA-Pancreatic
- ANAHATA-Thymus
- VISHUDDHA-Thyroid
- AJNA-Pituitary
- SAHASRARA- Pineal
Mawimbi ya Ubongo kwa sekunde
Mantra hizo zipo za aina nyingi na kugawanywa katika masomo au “Lessons”tofauti ambazo husababisha mawambi ya fikra kutulia katika ngazi tofauti za fikra za mwanadamu kama itavyoonyeshwa hapa chini.
Kupitia utafiti wa kisayansi, hamna ubishi wala upinzani kabisa kuhusu somo hili hasa katika dunia ya kwanza kimaendeleo. Pia kupitia utafiti uliofanywa nchini Afrika ya Kusini, hakuna budi nchi zingine za Afrika zijitahidi na kupendekeza utafiti wa aina hii katika magereza za ulinzi wa hali ya juu na kupunguza fujo au ukatili wa vurungu ndani ya jela hizo na kuleta amani kwa wafungwa.
BETA WAVES: “Ubongo Kawaida” Ubongo usio na utulivu mzuri na amani. Ubongo wenye Mizunguuko ya mawimbi 13 kwa sekunde
ALPHA WAVES:”Ubongo Tulivu na Makini” Mawimbi 8 kwa sekunde
THETA WAVES: “ Ubongo wenye ubunifu wote, furaha na amani” Mawimbi 4 kwa sekunde
DELTA WAVES: Ubongo wenye utabiri wa baadae na upeo wa kuona mengi mwanadam wa kawaida hayaweziona” Wimbi 1 kwa sekunde
**Imetoka kwenye majarida ya mwalimu wa Yoga, Instructor Fundi Rumadha
Mkufunzi wa sanaa ya Yoga toka “College of Neo- Humanistic Studies”, Sweden na Calcutta, Tiljala ,West Bengal, India.**
3 comments:
Namaskaram Acharya Rasadevanandaji( Sensei Fundi)!!Dhyana Sadhana.
One of few from Africa with that rank of Avadhuta in Tantrika Sadhana from Guruji Shrii Shrii Ananda Murtiji.Keep on teaching the people for tranquility and peace of mind over matter beyond the Superconscious Mind Sensei!! Oldest friend, Namaskar dadaji!!!
Namaskaram Acharya Rasadevanandaji( Sensei Romi Fundi)
Ni Mwafrika na mtanzania wa kwanza kukubalika katika hekalu
la Yoga na kupewa dhamana baraza la Guru's Calacutta,Bengal West India.
Inaonyesha wazi jinsi gani taifa lilivyoshindwa kuwatumia wataalamu kama huyu na wengineo.
Ana utalaamu gani wa kutumiwa na Taifa? Taifa halina dini, yoga ni dini kama ulivyothibitisha mwenyewe kuwa kakubalika katika hekalu.
Ndugu mzalendo acha wananchi waendelee na dini zao, usiwalazishe waikubali hiyo dini yako.
Ahsante.
Post a Comment