ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 31, 2017

MTANDAO MPYA WA VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII WASAJILIWA NCHINI

Mtandao mpya unaoundwa na Radio na vyombo vya habari vya kijamii Tanzania chini ya shirika la vyombo vya habari vya maudhui ya kijamii uliosajiliwa kwa jina la TANZANIA DEVELOPMENT INFORMATION ORGANIZATION-TADIO umeanzishwa rasmi baada ya kuvunjika kwa mtandao wa zamani wa COMNETA. Tukio hilo limetokea Julai 28, 2017 katika mkutano mkuu wa kwanza ambao pamoja na mambo mengine ulichagua safu mpya ya viongozi wa mtandao huo. Shirika la mtandao wa vyombo vya habari jamii Tanzania uliokuwa na jina la COMMUNITY MEDIA NETWORK OF TANZANIA – COMNETA, limevunjika rasmi mwezi machi mwaka huu. Katika mkutano huo kuwa kuundwa kwa shirika hilo jipya kunalenga kuhakikisha kunakuwa na mtandao makini wa Radio na vyombo vingine vilivyojikita katika kuibua kwa kuandika na kutangaza masuala ya kijamii kwa ajili ya maendeleo. 
Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe wakati wa mkutano huo.

Akihutubia katika mkutano huu kaimu mkuu wa ofisi ya UNESCO Tanzania, ambao ni wafadhili wakubwa wa mtandao huo Bw. Christophe Legay kwa niaba ya Mkuu wa ofisi Bi. Zulmira Rodrigues amepongeza hatua iliyofikiwa na Radio wanachama ya kuunda mtandao mpya. Alieleza kuwa UNESCO itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na shirika hilo jipya la TADIO ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma sahihi za kihabari zitakazosaidia kuboresha maisha yao na kuchochea maendeleo ya upashanaji wa habari nchini. Bw. Christophe amehimiza kwamba vyombo vya jamii vinao wajibu mkubwa wa kuhakikisha sauti za watu wanaowahudumia hasa wanaoishi vijijini.
Mwenyekiti mpya waTADIO Bw. Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe mara baada ya uchaguzi. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya TADIO, Maimuna Msangi na Katibu Mtendaji wa TADIO, Marco Mipawa.[/caption] Aliwaasa kushughulika na masuala ya kibinadamu na si watu binafsi. Wakati huo huo Mtandao huo unaoundwa na jumla ya Radio 32 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar, umefanya uchaguzi mkuu na kuwapata viongozi watakaosimamia shughuli zake kwa miaka mitatu ijayo. Uchaguzi huo ulitanguliwa na tukio la kujiuzuru kwa viongozi wa mpito waliochaguliwa mwezi Machi mwaka huu, baada ya kutangazwa rasmi kuvunjika kwa muungano wa awali wa radio jamii wa COMNETA. Katibu Mtendaji mpya wa TADIO, Marco Mipawa (kulia) akizungumza jambo mara baada ya uchaguzi kufanyika. Kutoka kushoto ni Balozi Mstaafu Mh. Christopher Liundi, Mkuu wa idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay, Mwenyekiti mpya waTADIO Bw. Prosper Kwigize na Mjumbe wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi.
Akitangaza matokeo, msimamizi wa uchaguzi huo ambae pia ni mlezi wa ushirika huo, Balozi mstaafu Mheshimiwa Christopher Liundi, alimtangaza Bw. Prosper Kwigize aliyekuwa mgombea pekee kuwa Mwenyekiti mpya baada ya kupata kura za ndiyo 26 kati ya kura 30 zilizopigwa na wajumbe waliohudhuria. Balozi Liundi, pia alimtangaza Bw. Marco Mipawa kuwa Katibu Mtendaji baada ya kupata kura 28 za ndiyo, Aidha Mipawa pia alikuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo. Viongozi wengine waliochaguliwa ni pamoja na Mweka Hezina, Shaaban Ali Makame aliepata kura 24 za ndiyo. Pia mkutano huo uliwachagua wajumbe sita wa Bodi ya shirika hilo la TADIO ambao ni Maimuna Msangi kutoka Pangani FM, Gladys Mapeka kutoka Radio Kilosa, Ali Mbarouk Omar kutoka kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari wa Pemba (PPC), Ali Khamis kutoka Adhana FM Zanzibar, John Baptist kutoka Dodoma FM na Anthony Masai kutoka Triple A FM. Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi (kulia) akimpongeza akimpongeza Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize.[/caption] Akizungumza baada ya kutangaza matokea hayo, Balozi Liundi aliitaka safu ya uongozi mpya kuongoza kwa kufuata katiba na malengo ya shirika hilo kwa lengo la kutetea maslahi mapana ya wananchi kwa kupitia kazi zinazofanywa na radio za kijamii. Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya wa TADIO Bw. Prosper Kwigize amewashukuru wajumbe kwa kuchagua safu mpya ya uongozi na kuahidi kujenga ushirikiano mpya ambao utawezesha kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa kwa mtandao huo wa ushirikiano wa vyombo vya habari vya kijamii. Bw. Kwigize ametoa wito kwa wadau wengine hususani Radio za kitaifa, magazeti, waandishi wa habari za mitandaoni (bloggers) Muungano wa wamiliki wa vyombo vya habari MOAT, TAMWA, MISA, Baraza la Habari Tanzania, Runinga na Vilabu vya waandishi wa habari mikoani kushirikiana na shirika la TADIO ili kutoa huduma stahiki kwa jamii. Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi akimpa pongezi Katibu wa TADIO Bw. Marco Mipawa (shati la kitenge) mara baada ya matokeo kutangazwa.

Amehimiza pia serikali na taasisi zake kutoa ushirikiano kwa TADIO ili misimamo, dira na malengo yanayoibuliwa na serikali yawafikie wananchi kwa haraka kupitia muungano huo wa Radio za mikoani. Amesisitiza kuwa, mtandao huo wa TADIO una ofisi na studio ya kisasa ndani ya Chuo Kikuu Huria Tanzania – OUT makao makuu Kinondoni Dar es Salaam ambako kazi ya ofisi na studio hiyo ni kuratibu shughuli za mtandao pamoja na kuandaa vipindi ambavyo vitakuwa vikisambazwa kwa radio wanachama. Aliitaka safu ya uongozi mpya kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kujenga umoja na mshikamano pamoja na kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuyafikia malengo ya ushirika huo. Mtandao wa TADIO unafadhiliwa na UNESCO chini ya mradi wa SIDA/SDC. Msimamizi wa uchaguzi huo mwanasheria Harold Sungusia (mwenye tai) akimpongeza Mwenyekiti mteule wa TADIO, Prosper Kwigize. Picha ya pamoja ya viongozi wa TADIO, Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi na Msimamizi wa uchaguzi huo Mwanasheria Harold Sungusia.

No comments: