ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 31, 2017

TANZIA: MUME WA MBUNGE MARY NAGU AFARIKI DUNIA


Dk Mary Nagu.
Profesa Joseph Nagu ambaye ni mume wa Mbunge wa Jimbo la Hanang mkoani Manyara, Dk Mary Nagu amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akidhibitisha kifo cha mume wake, Dk Nagu amesema kwamba marehemu alikuwa akipatiwa matibabu Muhimbili kwa zaidi ya mwezi mmoja na jana alifariki dunia saa 12 jioni.

Alisema mume wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa figo na moyo kwa muda mrefu. GPL

No comments: