Ofisi ya Bunge leo imeeleza kuwa Spika Job Ndugai amepokea barua kutoka kwa Maalif Seif Sharif Hamad yenye maelezo ya kuwafuta uanachama wabunge wawili Magdalena Hamis Sakaya na Maftaha Abdallah Nachuma akidai wamekosa sifa ya kuendelea na Ubunge.
Taarifa ya ofisi ya Bunge imeeleza kuwa ofisi ya Spika inayo barua ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha CUF Prof. Ibrahim Lipumba yenye kumbukunbu namba CUF/AK/DSM/MKT/05/2017 ya March 22, 2017 ikiliarifu Bunge kuwa Maalim Seif ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama Katibu Mkuu hivyo kwa mujibu wa Katiba ya CUF, majukumu ya Katibu Mkuu yatatekelezwa kuanzia tarehe hiyo na Magdalena Sakaya(MB).
Soma taarifa kamili:
No comments:
Post a Comment