ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 21, 2017

GRACE MUGABE AREJEA ZIMBAMWE KIMYA KIMYA BAADA YA KUKUMBU NA TUHUMA ZA KUMERUHI MTU AFRIKA KUSINI

Mke wa rais wa Zimbabwe, Garce Mugabe amerejea nchini Zimbabwe akitokea Afrika Kusini licha ya tuhuma za kumdhuru mwanamke mmoja kwenye hoteli Jijini Johannerburg.

Grace Mugabe mwenye umri wa miaka 52, amewasili Jijini Harare mapema leo kwa mujibu wa radio moja ya Zimbabwe, licha ya kuwepo kwa jitihada za kumzuia Afrika Kusini.

Mwanamitindo Gabriella Engels akiwa na plasta kichwani katika eneo aliloumia baada ya kupigwa na Grace Mugabe

Grace alikuwa anapaswa kuhudhuria mkutano siku ya jumamosi nchini Afrika Kusini lakini hakutokeza. Pia inadaiwa aliomba kupatiwa kinga ya Kidiplomasia.

Mama Mugabe anatuhumiwa kumpiga kwa waya wa umeme mwanamke mmoja mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20 kichwani na kumjeruhi.

No comments: