Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun mwenye makazi yake mjini Maputo,Msumbiji , Wawekezaji wa Uzalishaji Sukari na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi wa Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun mwenye makazi yake mjini Maputo,Msumbiji mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake Ikulu jijini Dar Es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi wa Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun mwenye makazi yake mjini Maputo,Msumbiji aliyeongozana na Wawekezaji wa Uzalishaji Sukari ambao wameonyesha utayari wa kuwekeza nchini Tanzania.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun mwenye makazi yake mjini Maputo,Msumbiji aliyeongozana na Wawekezaji wa Uzalishaji Sukari ambao wameonyesha nia na utayari wa kuwekeza nchini.
Mbali ya ujumbe kutoka Mauritius, wengine waliohudhuria mazungumzo hayo ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio .
Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais amewahakikishia wawekezaji hao ushirikiano wa Serikali na kuwaeleza kuwa Tanzania ina mazingira bora ya uwekezaji.
Mbali ya fursa ya uwekezaji katika Sukari, Makamu wa Rais aliainisha maeneo mengine ya kuwekeza kama vile viwanda na TEHAMA.
Aidha alisema pindi uwekezaji huo ukifanikiwa , Tanzania itafaidika na soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na masoko mengine duniani kwa ujumla.
Uwekezaji huu utakuwa wa Ubia kati mashirika ya hifadhi ya mifuko ya jamii na pia kampuni nyingine za wazawa.
No comments:
Post a Comment