Leo nimemua kuzungumzia suala ambalo wapenzi wengi limekuwa likiwatesa hasa wanawake.
Kufikia kilele cha Mlima Kilimanjaro au kufika mshindo, kuridhishana mnapokuwa faragha, penzi ni tamu kama ukimpata anayeyajua mapenzi, kisha mkaridhiana, mkaelewana hakika mtayafurahia mapenzi yenu.
Wanaume wengi huweza kufurahia tendo la ndoa wanapokuwa na wenza wao, kuliko wanawake, wanaume wanaweza kufikia mshindo kwa haraka zaidi kuliko wanawake.
Wakati idadi kubwa ya wanaume ikiongoza kwa kufikia mshindo, wanawake wengi zaidi hushindwa kufurahia tendo hilo na kuishia hewanihewani.
Kama nilivyosema awali, mapenzi ni kuridhiana, kuelewana, kukubaliana sasa inapotokea mko faragha halafu mmoja wapo anafurahia na mwingine anaishia kunukia shombo ya mchezo si sawa.
Na mbaya zaidi anayeishia kugugumia kwa maumivu anachukuliwa poa, eti alishazoea. Hili ni tatizo tena kubwa ambalo linaweza kusabisha usaliti katika uhusiano wenu.
Tatizo hili linaweza kukufanya uanze kuwaza namna ya kuchepuka ili kutafuta tamu ya penzi au wewe mwanaume unaweza kuwa chanzo cha mwenza wako kuchepuka.
Pamoja na kuwa wanawake wengi, hawajui raha ya mapenzi, bado akili za wengi zimetawaliwa na nidhamu ya woga wanapokuwa faragha.
Ni nadra sana kwa mwanamke ambaye hajafurahia penzi la mwenza wake kumuambia ukweli mpenzi wake kuwa hajaridhika kwa sababu zifuatazo:
ATAONEKANA NI MALAYA
Baadhi ya wanawake wanashindwa kuwaambia ukweli wapenzi wao pindi ambapo hawafurahii tendo la ndoa kwa kuhisi anaweza kuonekana ni malaya aliyekubuhu au ni mwanamke anaye-penda sana ngono kuliko kitu kingine.
Kwa mantiki hiyo, mwanamke huamua kupotezea na kubaki akigugumia kwenye mtima wake. Jambo ambalo ni hatari kwa uhusiano wake.
ANAONEKANA HANA ADABU
Wanawake wengine huona tu aibu kuzungumzia suala la faragha na mwenza wake kwa kuamini kuwa halipaswi kuzungumzwa. Anaona ni bora kufa na tai yake shingoni kuliko kusema ukweli.
Wewe mwanamke unayeona aibu kuzungumza na mwenza wako kuhusu kinachokusibu hasa mnapokuwa faragha unakosea kwa kuwa inawezekana mwenza wako hajagundua tatizo
hilo, yeye anahisi ni kidume cha mbegu kwa sababu anakufurahisha kumbe ukweli hujawahi kufurahia.
UKOROFI WA MWANAUME
Wakati mwingine mwanamke anaweza kuhofia kumwambia mwanaume kwa sababu ya tabia au ukorofi alionao.
Pengine huwa hasikilizi ushauri na maoni yake hivyo anaona hata jambo hilo akikuambia itakuwa yaleyale tu.
Kwa tabia hiyo ya kujiona yeye ni kila kitu bila kumpa nafasi mwenza wake, hukosa mambo mengi na mwisho wake hukaribisha michepuko kwenye penzi au ndoa.
Pamoja na mambo yote niliyoyazungumza hapo awali, fika sehemu mwanaume au mwanamke jiulize hivi kwa nini ukubali kuteseka na penzi wakati mpenzi wako unaye?
Kwa nini ufikirie kuchepuka wakati unaweza kuzungumza na mpenzi wako na akawa bora zaidi?
Kwa ushauri; tembelea ukurasa wetu wa Facebook Page: Mimi na Uhusiano, Ista: mimi_na_uhusiano au jiunge na Mi&u kwenye WhatsApp kwa namba Maoni/Ushauri +255 679-979-785
GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake