ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 3, 2017

MPENZI WAKO HAKURIDHISHI? MFUNGUKIE BWANA!

KWANZA nimshukuru Mungu kwa kuni­jalia afya njema. Pia nikukaribishe msomaji wangu katika jamvi lako ulipendalo la UIimwengu wa Mahaba.

Leo nimemua kuzun­gumzia suala ambalo wapenzi wengi limekuwa likiwatesa hasa wanawake.

Kufikia kilele cha Mlima Kilimanjaro au kufika mshindo, kuridhishana mnapokuwa faragha, penzi ni tamu kama ukimpata anayeyajua mapenzi, kisha mkaridhiana, mkaele­wana hakika mtayafurahia mapenzi yenu.

Wanaume wengi huweza kufurahia tendo la ndoa wa­napokuwa na wenza wao, kuliko wanawake, wanaume wanaweza kufikia mshindo kwa haraka zaidi kuliko wanawake.

Wakati idadi kubwa ya wanaume ikiongoza kwa kufikia mshindo, wanawake wengi zaidi hushindwa kufurahia tendo hilo na kuishia hewanihewani.

Kama nilivyosema awali, mapenzi ni kuridhiana, kuelewana, kukubaliana sasa inapotokea mko faragha halafu mmoja wapo anafurahia na mwingine anaishia kunukia shombo ya mchezo si sawa.

Na mbaya zaidi anayeishia kugugumia kwa maumivu anachukuliwa poa, eti alishazoea. Hili ni tatizo tena kubwa ambalo linaweza kusabisha usaliti katika uhusiano wenu.

Tatizo hili linaweza kuku­fanya uanze kuwaza namna ya kuchepuka ili kutafuta tamu ya penzi au wewe mwanaume unaweza kuwa chanzo cha mwenza wako kuchepuka.

Pamoja na kuwa wa­nawake wengi, hawajui raha ya mapenzi, bado akili za wengi zimetawaliwa na nidhamu ya woga wana­pokuwa faragha.

Ni nadra sana kwa mwa­namke ambaye hajafurahia penzi la mwenza wake kumuambia ukweli mpenzi wake kuwa hajaridhika kwa sababu zifuatazo:

ATAONEKANA NI MALAYA


Baadhi ya wanawake wanashindwa kuwaambia ukweli wapenzi wao pindi am­bapo hawafurahii tendo la ndoa kwa kuhisi anaweza kuonekana ni malaya ali­yekubuhu au ni mwanam­ke anaye-penda sana ngono kuliko kitu kingine.

Kwa mantiki hiyo, mwan­amke huamua kupotezea na kubaki akigugumia kwenye mtima wake. Jambo am­balo ni hatari kwa uhusiano wake.

ANAONEKANA HANA ADABU

Wanawake wengine huona tu aibu kuzungumzia suala la faragha na mwen­za wake kwa kuamini kuwa halipaswi kuzungumzwa. Anaona ni bora kufa na tai yake shingoni kuliko kusema ukweli.

Wewe mwanam­ke unayeona aibu kuzungumza na mwenza wako kuhusu ki­nachokusi­bu hasa mnapokuwa faragha unakosea kwa kuwa inawezeka­na mwenza wako hajagund­ua tatizo

hilo, yeye anahisi ni kidume cha mbegu kwa sababu anakufurahisha kumbe uk­weli hujawahi kufurahia.

UKOROFI WA MWANAUME

Wakati mwingine mwa­namke anaweza kuhofia kumwambia mwanaume kwa sababu ya tabia au ukorofi alionao.

Pengine huwa hasikili­zi ushauri na maoni yake hivyo anaona hata jam­bo hilo akikuambia itakuwa yaley­ale tu.

Kwa tabia hiyo ya kujiona yeye ni kila kitu bila kumpa nafasi mwenza wake, hukosa mambo mengi na mwisho wake hukaribisha michepuko kwenye penzi au ndoa.

Pamoja na mambo yote niliyoyazungumza hapo awali, fika sehemu mwa­naume au mwanamke jiulize hivi kwa nini ukubali kuteseka na penzi wakati mpenzi wako unaye?

Kwa nini ufikirie kuchepu­ka wakati unaweza kuzun­gumza na mpenzi wako na akawa bora zaidi?

Kwa ushauri; tem­belea uku­rasa wetu wa Face­book Page: Mimi na Uhu­siano, Ista: mimi_na_uhu­siano au jiunge na Mi&u kwenye WhatsApp kwa namba Maoni/Ushauri +255 679-979-785

GPL

No comments: