JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Anwani ya simu:“MAKAMU”, Mji wa Serikali, Simu Na.: +(255)026 2329006 Eneo la Mtumba, Nukushi.: +(255)026 2329007/2983150 S. L. P. 2502, Barua Pepe: km@vpo.go.tz 40406 DODOMA, TANZANIA.
06 Januari 2025
Accra - Ghana
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 06 Januari 2025, amewasili Jijini Accra nchini Ghana ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho wa Rais Mteule wa Ghana Mhe. John Dramani Mahama.
Uapisho wa Rais Mteule wa Ghana Mhe. John Mahama utafanyika kesho tarehe 07 Januari 2025 katika Uwanja wa Independence Square Jijini Accra.
Franco Singaile
Msaidizi wa Makamu wa Rais - Habari
No comments:
Post a Comment