ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 21, 2017

Mzee Kilomoni – Mimi bado mwanachama wa Simba SC

Mbali na taarifa za kuondolewa kwenye bodi ya wadhamini wa klabu ya Simba na kusimamishwa uanachama wa klabu hiyo huku akipewa sharti la kufuta kesi aliyofungua mahakamani, Mzee Hamis Kilomoni hana habari na masharti hayo na ameendelea kukomaa kuwa hatafuta kesi hiyo mahakani kwani hajapata barua ya kufukuzwa uanachama.

Kupitia Mkutano mkuu wa Simba uliofanyika wiki mbili zilizopita klabu hiyo iliamua kumuondoa Hamisi Kilomoni katika bodi ya wadhamini na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Mgoyi huku kaimu rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah akieleza Kilomoni kusimamishwa uanachama hadi atakapofuta kesi mahakamani huku akiutanabaisha umma kuwa asipofanya hivyo watamfuta uanachama moja kwa moja.
Nangoje barua ya uamuzi huo, ninachojua mimi bado niko Simba kwa kuwa sijapewa barua rasmi hadi sasa, Siwezi kulizungumzia kwa kina sababu sina barua, nitakapoletewa barua rasmi ndipo nitakuwa katika nafasi ya kulizungumzia,“amesema Mzee Kilomoni kwenye mahojiano yake na gazeti la Mwanaspoti.
Kuhusu taarifa za yeye kufuta kesi mahakamani, Kilomoni alisema hajafuta na hawezi kufanya hivyo hivi sasa ingawa hakutaka kuzungumzia kama atakuwa tayari kufuta kesi endapo ataletewa barua hiyo.
Narudia tena nikishapewa barua rasmi nitakuwa kwenye nafasi ya kuzungumza kila kitu, najua klabu yetu ina matatizo mengi, lakini yote tuyaache kwanza nisubiri barua yangu ya kusimamishwa kwanza,“amesema Kilomoni.
Hata hivyo, klabu ya Simba leo Jumapili itakuwa na mkutano wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo mkutano utakaofanyika jijini Dar es Salaam, huenda ikalijadili kwa mara nyingine sakata la Kilomoni.

No comments: