ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 25, 2017

SHIRIKA LA WOTESAWA LATAMBULISHA AWAMU YA PILI YA MRADI WA KUWALINDA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI

Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTESAWA, Angel Benedicto, akitoa mrejesho wa awamu ya kwanza ya mradi wa kulinda na kutetea haki na maslahi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani uliokuwa ukiendeshwa kwenye Kata nne Jijini Mwanza kwa muda wa miezi sita. Awamu ya kwanza ya mradi huo ilitekelezwa vyema na hivyo kufungua milango ya mwendelezo wa mradi wa awamu ya pili utakaodumu kwa miaka miwili kwenye Kata sita Jijini Mwanza. Mmoja wa washiriki akitoa pongezi kwa Shirika la WOTESAWA kwa kazi nzuri ya kutetea haki na maslahi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani na pia kuuliza maswali na kuchangia mada kwenye semina hiyo Baadhi ya washiriki wa semina hiyo iliyowahusiusha Maafisa Kazi, Ustawi wa Jamii, madiwani, jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia, wenyeviti wa serikali za Mitaa pamoja na Waandishi wa Habari
Baadhi wa washiriki wa semina ya utambulishi wa mradi wa kuwalinda na kuwatetea watoto wafanyakazi wa nyumbani iliyofanyika hii leo Jijini Mwanza, chini ya Shirika la WOTESAWA. Baadhi ya washiriki wa semina hiyo iliyowahusiusha Maafisa Kazi, Ustawi wa Jamii, madiwani, jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia, wenyeviti wa serikali za Mitaa pamoja na Waandishi wa Habari. Mratibu wa Shirika la Kutetea Haki za Wafanyakazi wa Nyumbani (Wotesawa), Elisha Daudi, akifuatilia kwa umakini mrejesho kuhusu awamu ya kwanza ya mradi wa kuwalinda na kutetea haki na maslahi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani Jijini Mwanza, uliowasilishwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo, Angel Benedicto. Baadhi ya washiriki Baadhi ya washiriki wa semina hiyo iliyofanyika leo Jijini Mwanza. Baadhi ya washiriki wa semina hiyo iliyowahusiusha maafisa kazi, ustawi wa jamii, madiwani, jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia, wenyeviti wa serikali za Mitaa pamoja na Waandishi wa Habari ambapo Shirika la WOTESAWA limetoa mrejesho wa awamu ya kwanza ya mradi wa kulinda na kutetea haki na maslahi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani uliokuwa ukiendeshwa kwenye Kata nne Jijini Mwanza kwa kipindi cha miezi sita. Mradi huo ulitekelezwa vyema na hivyo kufungua milango ya awamu ya pili ya mradi wa aina hiyo utakaotekelezwa kwenye Kata sita Jijini Mwanza kwa kipindi cha miaka miwili.
BMG Habari, Pamoja Daima!

BMG Habari, Pamoja Daima! Shirika la Kutetea Haki na Maslahi ya Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTESAWA lenye makazi yake Jijini Mwanza, limetambulisha awamu ya pili ya mradi wa kuzuia ukatili kwa watoto hao na kulinda haki na maslahi yao. Kabla ya kutambulishwa kwa mradi huo, shirika hilo lilitoa mrejesho wa mradi wa aina hiyo awamu ya kwanza uliokuwa ukiendeshwa kwenye Kata nne Jijini Mwanza, uliodumu kwa kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi Oktoba mwaka jana hadi mwezi Aprili mwaka huu. Akiwasilisha mrejesho huo hii leo Jijini Mwanza, Mkurugenzi wa shirika la WOTESAWA, Angel Benadicto amesema awamu ya kwanza ya mradi huo ilifanikiwa vyema na hivyo kuwezesha upatikanaji wa awamu ya pili ya mradi wa aina hiyo kutoka kwa wafadhiri ambao ni shirika la The Foundation For Civil Society. “Wao wanasema ni muda mwafaka wa kutokomeza ukatili kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani ambapo sasa tutakuwa kwenye Kata sita Jijini Mwanza”. Amesema Benedicto. Amesema kwa awamu ya kwanza, watoto wafanyakazi wa nyumbani 154 pamoja na waajiri 199 walifikiwa na kujengewa uelewa ili kuzuia ukatili dhidi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani ambapo mafunzo kama hayo pia yaliwafikia wadau mbalimbali kama polisi kupitia dawati la jinsia, vyombo vya habari, watendaji wa serikali wakiwemo madiwani na wenyevyiti wa mitaa. Aidha elimu ya aina hiyo imesambaa zaidi katika jamii kupitia vipindi 15 vilivyorushwa redioni, vipindi saba vilivyorushwa kwenye luninga pamoja na machapicho mbalimbali ambapo wajiri na waajiriwa wao 25 walisaini mikataba ya ajira. Mratibu wa Shirika la Kutetea Haki za Wafanyakazi wa Nyumbani (Wotesawa) Elisha Daudi, amesema matarajio ya mradi huo ni kuhakikisha ukatili dhidi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani unatokomezwa katika jamii na pia kutoa fursa kwa watoto kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu. 

No comments: