Advertisements

Saturday, August 5, 2017

SMZ YAOMBOLEZA KIFO CHA MWANASIASA MKONGWE NCHINI, MZEE JOHN LISA CHIPAKA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Picha na – OMPR – ZNZ.
 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa mkono wa pole kwa Chama cha 
Siasa cha ADATADEA Taifa kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa Chama hicho
Mzee John Lisa Cipaka.

Salamu hizo zimewasilishwa na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Wazizi asiye na Wizara Maalum wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Mh. Juma Ali Khatibu wakati wa mazishi ya Mwanasiasa huyo Mkongwe Tanzania yaliyofanyika leo mchana katika Makaburi ya Kinondoni Jijini
Dar es salaam.

Mh. Juma Ali Khatibu amemuwakilisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye msiba huo uliogusa nyoyo za Wanachama wa
Chama cha ADATADEA pamoja na Watanzania walio wengi Nchini.

Mzee John Lisa Chipaka ni miongoni mwa Wanasiasa wakongwe Nchini Tanzania waliotoa mchango mkubwa katika harakati za Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya Siasa mnamo mwaka 1992.

Katika harakati za kisiasa Mzee Chipaka alikuwa Mjumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania nafasi aliyoitumikia kwa juhudi na umahiri
mkubwa hadi kufariki kwake.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wananchi wa Zanzibar wameupokea kwa huzuni msiba huo na kuwataka Wanachama wa ADATADEA pamoja na
familia ya Marehemu kuwa na moyo wa subira katika kipindi hichi cha msiba.

Mwenyezi Muungu ailaze royo ya Marehemu Mzee John Lisa Chipaka mahali pema peponi. Amin.
 
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments: