Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari na wahariri wa vyombo mbalimbali waliokutanishwa ili kujadili namna ya kufanya kazi katika Tamasha la 14 la Kijinsia litakalofanyika Septemba 5 hadi 8 mwaka huu katika Ofisi za Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam.
TGNP Mtandao kutambua mchongo wa wanawake walioshiriki kuleta maendelea nchini hapa nchini Tanzania katika Tamasha la 14 la Kijinsia litakalofanyika Septemba 5 hadi 8 mwaka huu katika Ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam.
Akizungumza na katika semina ya kutoa elimu juu ya tamasha hilo kwa Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Lihundi, alisema lengo la tamasha hilo ni kusherehekea, kujadili changamoto na mafanikio ya harakati wanazozifanya.
Alisema Tamasha hilo litawahusisha wanawake mbalimbali ambao wamepata mafanikio makubwa katika harataki za ukombozi wa mwanamke na kuhakikisha usawa wa kijinsia.
“Katika siku zote nne wanawake zaidi ya 1000 watakaa na kujadili changamoto zinazoikumba jamii, kusherekea mafanikio yaliyopatikana na kujenga nguvu ya pamoja katika kuhakikisha ukatili wa kijinsia unaisha.
“Kutokana na kauli mbiu ya tamasha hili inavyosema kuwa Mageuzi ya Mfumo Kandamizi kwa Usawa wa Kijinsia na Maendeleo. Tunakata kuangalia mwanamke anaonekana vipi katika hazma ya Serikali kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda,” alisema Lilian.
Aidha alisema wajasilimali wataonesha bidhaa na kupata elimu ya namna gani wanaweza kuboresha bidhaa zao na ufungashaji ili waweze kuingia kwenye soko la ushindani la bidhaa za ndani na nje ya nchi kutoka Shirika la Viwanda vidogo (Sido), Mamlaka ya Chakula a Dawa (TFDA) na Taasisi ya Udhibiti Ubora (TBS) kwa ajili ya kupewa.
Balozi Getrude Mongella akizungumza na waandishi pamoja na wahariri wa vyombo vya habari leo kuhusu maandalizi ya Tamasha la 14 la Kijinsia litakalofanyika Septemba 5 hadi 8 mwaka huu katika Ofisi za Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam.
Afisa Program uchambuzi na Machapisho kutoka TGNP Mtandao, Bw. Deogratius Temba akizungumza jambowakati wa semina iliyowakutanisha waandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali uliondaliwa na TGNP Mtandao.
Baadhi ya wahariri pamoja na wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakiwa kwenye semina
Afisa Habari wa TGNP Mtandao,Monica John akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari waliofika kwenye semina iliyokuwa inahusu tamasha la wanawake litakalofanyikaTGNP Mtandao
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakichangia mada kwenye semina iliyowakutanisha ili kujadili namna nzuri ya kufanya kazi katika Tamasha la 14 la Kijinsia litakalofanyika Septemba 5 hadi 8 mwaka huu katika Ofisi za Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam.
Picha ya Pamoja
No comments:
Post a Comment