Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akifungua semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali kujadili ripoti ya utafiti ya uboreshaji wanawake kiuchumi nxhini Tanzania kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Profesa Frola Kessy kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha ripoti ya utafiti kuhusu uboreshaji wa wanawake kiuchumi nchini Tanzania kwenye mkutano uliofanyika leo katika hoteli ya Protea Courtyard na kuandaliwa na TGNP Mtandao.
TGNP Mtadao wakishirikiana na wadau mbalimbali wamefanya uchambuzi wa utafiti na sera kwa ajili ya ukombozi wa mwanamke kiuchumi.
Akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi amesema ili kumkomboa mwanamke kiuchumi lazima kuangalia na mazingira yanayomzunguka, kwani huwezi kumkomboa mwanamke wakati bado ukatili wa kijinsia unaendelea, bado mwanamke anatumia muda mwingi kutafuta maji na hata wanapokwenda hospitalini wanatumia muda mwingi kutokana na kukosekana kwa huduma ya mama na mtoto.
Hivyo leo wamewakutanisha wadau mbalimbali kutoka serikalini, taasisi binafsi pamoja na wabunge ili kuchambua sera pamoja na utafiti uliofanywa na TGNP Mtandao ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili wanawake hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Profesa Frola Kessy kutoka TGNP Mtandao amesema sera nyingi zina masuala ya usawa wa kijinsi lakini tatizo linakuwa kwenye utekelezaji wa sera hizo. Amesema kuwa bajeti inayopangwa hasa kwenye masuala ya ustawi wa jamii zinaweza kuja au hata zikija ni ndogo sana ambazo haziwezi kutatua matatizo ya wanawake nchi nzima.
Baadhi ya wadau wa kutetea haki za wanawake wakiwa kwenye mkutano uliowakutanisha kujadili matokeo ya utafiti ya uboreshaji wanawake kiuchumi leo jijini Dar es Salaam.
Geofrey Chambua akifafanua jambo kwenye semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali ili kujadili utafiti na sera ili kuboresha wanawake kiuchumi nchini Tanzania.
Mkutano ukiendelea
Baadhi ya Makundi yakijadili yakijadili utafiti uliofanywa na TGNP Mtandao ili kuja na mapendekezo yatakayoweza kumwinua mwanamke Kiuchumi kwenye mkutano ulioandaliwa na TGNP Mtandao leo jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Busanda Mkoani Geita Lolensia Bukwimba akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa kutetea haki za wanawake ili kujadili sera pamoja na tafiti zilizofanywa kuhusumwanamke na maendeleao ya taifa
kiujumla.
Profesa Frola Kessy kutoka TGNP Mtandao akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye mkutano uliowakutanisha wadau wa kutetea wanawake
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake