ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 21, 2017

WIZARA ZAUNGANA KUDHIBITI UHALIFU BARABARANI KWA NJIA YA KAMERA

 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto waliokaa)   na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Gillard Ngewe ,walipotembelea kituo cha kufuatilia mwenendo wa mabasi, kilichopo jijini Dar es Salaam,  ikiwa katika Mpango wa Wizara hizo kushirikiana katika kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia mifumo maalumu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mtaalamu wa Mifumo ya Komputa kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Godfrey Nsato, akifafanua jinsi Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi unavyofanya kazi kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto waliokaa) na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, walipotembelea Kituo cha Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi,kilichopo jijini Dar es Salaam, ikiwa katika Mpango wa Wizara hizo kushirikiana katika kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia mifumo maalumu.
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kutembelea Kituo cha   Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi, kilichopo  jijini Dar es Salaam, ikiwa katika Mpango wa Wizara hiyo kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia mifumo maalumu.
 Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kutembelea Kituo cha Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi, kilichopo   jijini Dar es Salaam, ikiwa katika Mpango wa Wizara hiyo kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia mifumo maalumu.
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu  kulia),Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhandisi Edwin Ngonyani(wapili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, baada ya kumaliza kutembelea Kituo cha   Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi,kilichopo  jijini Dar es Salaam.Wengine waliokaa Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa SUMATRA, Hilda Gondwe na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA),Gillard Ngewe.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Gillard Ngewe (Kushoto), baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Kituo cha Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi, kilichopo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano   Mhandisi Edwin Ngonyani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments: