Ofisi ya Bunge imetoa uthibitisho wa nyaraka kuonyesha kuwa fedha zilizochangwa na wabunge zimewasilishwa hospitalini anakotibiwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Lissu aliyeshambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma Septemba 7, anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
“Napenda kusisitiza kuwa fedha zilizochangwa na wabunge Sh43 milioni kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mheshimiwa Tundu Lissu tayari zimetumwa katika Akaunti ya Hospitali ya Nairobi anakopatiwa matibabu,” imesema taarifa iliyotolewa leo Jumapili na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano cha Bunge.
Fedha hizo zimetumwa kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Bunge limesema fedha hizo ambapo kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya BoT kwa siku hiyo ili kuwa ni sawa na Shilingi ya Kenya 1,977,120.58.
“Kiasi hicho cha Fedha kilitumwa Septemba 20, 2017 kwenda Benki ya Barclays, Tawi la Hurlringham, Akaunti Namba 0451155318 yenye jina la Kenya Hospital Association.
No comments:
Post a Comment