Dar es Salaam. Hizi ndizo kauli zilizotolewa na viongozi kuhusu matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema), Tundu Lissu baada ya kupelekwa jijini Nairobi.
Katika kauli hizo Spika wa Bunge, Job Ndugai anaeleza kuwa utaratibu wao wa kumpeleka Lissu nje ni lazima apitie Muhimbili kwa kuwa Bima ya Afya ndivyo inavyotaka.
Hata hivyo, Mbunge wa Iringa Mjini(Chadema), Mchungaji Peter Msigwa anasema kuwa bima walizo nazo wabunge hazifanyi kazi nje ya nchi ndiyo maana hata Kenya wamewashangaa.
Lakini Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu hivi sasa anasema Serikali iko tayari kumtibia Lissu mahali popote duniani. Sasa swali la kujiuliza utaratibu ni upi?
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment