Advertisements

Monday, September 18, 2017

UPELELEZI KESI YA AVEVA, KABURU UMEKAMILIKA

Upelelezi wa awali katika kesi ya utakatishaji fesha inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa leo September 18, 2017 kuwa, upelelezi wa awali wa kesi hiyo umekamilika ambapo jalada la kesi limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili alisome na kueleza kama anaona umekamilika au la.

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi September 27, 2017.

Aveva na Kaburu wanashtakiwa na TAKUKURU wakikabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha fedha kiasi cha dola za Marekani 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.

Upelelezi uliokuwa unafanyiwa kazi ni nyaraka za kughushi maandiko zilizokuwa zimepelekwa kwa mtaalam kufanyiwa uchunguzi ili kubaini makosa hayo.

No comments: