Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Grolius Luoga akizungumza na watoto wakati wa kongamano la kuzuia mimba za utotoni kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yanayofanyika tarehe 11 Oktoba 2017 katika wilaya ya Tarime mkoani Mara.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai akiwasalimia watoto waliojumuika kwenye kongamano la kuwajengea watoto uelewa wa kujilinda dhidi ya ndoa za utotoni siku moja kabla ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Kitaifa yanayofanyika tarehe 11 Oktoba, 2017 wilaya ya Tarime mkoani Mara.
Mwakilishi wa watoto wilayani Tarime Anna Simon akiwakilisha watoto wa wilaya ya Tarime kutoa salamu za watoto kwa Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw. Glorius Luoga(hayupo pichani) wakati wa mjadala wa ulinzi wa watoto katika ngazi ya familia, shuleni, mtaani na jamii kwa ujumla.
Baadhi ya watoto, wazazi, walezi na wazee wa mila katika wilaya ya Tarime wakifuatilia kwa makini nasaha za Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Grolius Luoga(hayupo pichani) kuhusu wajibu wa kuwalinda watoto dhidi ya mimba za utotoni katika wilaya ya Tarime, mkoani Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Grolius Luoga akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa mwakilishi wa watoto Anna Simon mara baada ya kufungua kongamano la watoto wilaya ya Tarime, mkaoni Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Grolius Luoga akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa ulinzi na usalama wa mtoto katika ngazi ya jamii wilaya ya Tarime, mkoani Maramara baada ya kufungua kongamano la watoto.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
No comments:
Post a Comment