Katibu wa kampeni ya "mtoto kwanza elimu ni msingi" Atley T Kayuni akitoa somo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mabwegere iliyopo Kilosa Mkoani Morogoro kabla yakutoa msaada kwa wanafunzi hao.
Na MWandishi Wetu
Shirika lisilo la kiserikali la Rise charity limezindua kampeni iitwayo Mtoto kwanza Elimu ni Msingi Ambapo kampeni hiyo yenye dhumuni la kusaidia watoto wa shule za msingi kwa kuwachangia vifaa mbalimbali vitakavyo wawezesha katika Masomo .
Kampeni hiyo imezinduliwa kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Morogoro wilaya ya kilosa kijiji cha Ngoisani ndani ya shule ya Mabwegere ikiwa ni kampeni inayotarajiwa kuzunguka katika mikoa mbalimbali Tanzania.
Aidha wakati wa uzinduzi huo ulioambatana na kutoa msaada wa vifaa vya kujifunzia Katibu wa kampeni hiyo Atley Timothy Kayuni amewaasa watoto kwa kusema
"Msaada huu umetolewa na watanzania na wapenda maendeleo hivyo muutumie vizuri na kwamanufaa ya upataji elimu bora ambayo itawasaidia mbeleni katika maisha hivyo mkazane ili kutimiza ndoto zenu" amesema Kayuni
Naye Mmoja wa walimu katika shule hiyo Mwl. Mbapila amelishukuru shirika hilo kwa kuwakumbuka na kwenda kuwaona na kusema ni watu wachache sana wenyemoyo wa kujitolea hivyo wasichoke kutoa kwani shule ni nyingi na nyingi zinahari mbaya hususani vijijini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Rise Media, Innocent Horomo akitoa msaada wa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi, ikiwa ni kampeni inayoendeshwa na Rise Charity iliyofanyika katika shule ya shule ya Mabwegere wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
Afisa habari wa Rise Media ambae pia ni mwakilishi wa Rise Charity akiteta jambo na wanafunzi wa shule ya msingi mabwegere wakati wa zoezi la uzinduzi wa kampeni ya Mtoto kwanza elimu ni msingi
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mabwegele wakiwa darasani wakati wa zoezi la kampeni ya Mtoto kwanza elimu ni msingi.
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mabwegere akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Rise Charity kwa kuwakumbuka na kuwapa msaada
Wanafunzi wakifurahia msaada waliopewa kwa kunyosha juu vifaa vya kujifunzia
No comments:
Post a Comment