ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 16, 2017

SBL YAZINDUA MSIMU WA PILI WA ‘’SMIRNOFF ICE BLACK DJ SEARCH’’ NDANI YA MIKOA MITANO.

Meneja wa bidhaa wa SBL Ester Raphael akizungumza na vyombo vya habari kabla ya kuanza uzinduzi wa msimu wa pili wa kampeni ya ‘’SMIRNOFF ICE BLACK DJ SEARCH’’ Ambayo ilizinduliwa mapema mwishoni wa wiki iliyopita katika fukwe za Coco Jijini Dar es salaam na kuwakutanisha Madj 30 ambapo wanatafutwa Madj 10 kuingia Fainali.
Mmoja wa washiriki wa shindano la ‘’SMIRNOFF ICE BLACK DJ SEARCH’’ Akiwa katika mashine kuonesha ujuzi wake huku jaji mkuu DJ PQ akimsikiliza kwa makini mapema mwishoni wa wiki iliyopita katika fukwe za Coco. 
Washiriki wa shindano la ‘’SMIRNOFF ICE BLACK DJ SEARCH’’ Wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo inayoendeshwa katika mikoa mitano huku wakitafuta washindi watatu watakaoibuka na zawadi kutoka SBL 
Mmoja wa washiriki wa shindano la ‘’SMIRNOFF ICE BLACK DJ SEARCH’’ akiwa katika mashine kuonesha ufundi wake katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo mapema mwishoni wa wiki iliyopita katika fukwe za Coco Jijni Dar es salaam.
Baadhi ya mashabiki waliokuja kushuhudia uzinduzi wa kampeni ya ‘’SMIRNOFF ICE BLACK DJ SEARCH’’ wakifuatilia kwa makini washiriki wakionesha uwezo wao katika kuchanganya mziki mapema mwishoni wa wiki iliyopita katika fukwe za Coco Beach . 
Mshiriki wa shindano la ‘’SMIRNOFF ICE BLACK DJ SEARCH’ akionesha umahiri wake katika kutumia mashine mapema mwishoni wa wiki ikiyopita katika fukwe za Coco.

Dar es Salaam, Oktoba 14 2017-Kampuni  ya bia ya Serengeti (SBL) leo  imezindua upya  msimu wa pili wa ‘’Smirnoff ice black’’ (SIB) Dj search . Kampeni  hii  ya miezi mitatu itakayolenga kusaka Dj bora na kuleta karibu kinywaji hicho kwa watumiaji  wake nchi nzima.

Akiongea katika uzinduzi huo maeneo ya Coco Beach Dar es salaam Meneja wa bidhaa wa SBL Ester Raphael amesema mashindano haya yana dhumuni la kuhamasisha na kuvutia watumiaji wapya wa kinywaji hicho huku wakishindanisha maDJ nchi nzima na kupata vinara watatu ambao watapa ta zawadi nono.

Lengo jingine la uzinduzi huu alifafanua  Ester ‘’Ni kuongeza ufahamu wa kinywaji hicho kwa watumiaji wake kwamba ni kinywaji ambacho kipo tayari kwa kunywa na kuhamasisha kuwa ina ladha ya kipekee ya limao.

 “Tunaamini kwa kupitia shindano hili , SBL itatoa msisimko kwa wateja wake na muziki mzuri na nafasi ya kipekee kuonyesha uwezo wa MaDj wanaochipukia’’. Ester ametaja mikoa ambayo shindano hilo litafanyika, mikoa hiyo ni pamoja na Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Morogoro, and Mwanza kila mkoa kutoa maDj 10 na jumla kuwa maDJ 50, mwishoni watapambanishwa na kupata washindi watatu ambao watapokea zawadi kutoka SBL.

“Kutakuwa na zawadi kwa washindi wetu”, alifafanua na kusema zawadi hizo zitajumuisha DJ kits, laptops na controllers kwa washindi watatu watakaofika finali hizo.

Ester alimalizia kwa kusema “Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwaalika maDj wote na wapenzi wa muziki kujumuika nasi katika shindano hili ili kusherekea kwa pamoja na kinywaji chetu cha Smirnoff Ice Black’’

No comments: