ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 28, 2017

JAPAN YAONESHA NIA KUIJENGA DODOMA KWA MIUNDOMBINU YA KISASA

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazopata ufadhili mkubwa wa miradi mbalimbali ya maendeleo kutoka Japan kupitia Shirika hilo la Kimataifa la Maendeleo (JICA).


Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa barabara ya juu (fly over) katika eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam, upanuzi wa awamu ya kwanza ya barabara mpya ya Bagamoyo (Mwenge-Tegeta) na ufadhili mpya wa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hiyo kutoka Morocco hadi Mwenge.


Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase, pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (wa pili kulia) wakijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika Nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu, nishati, kilimo na maji, walipokutana Jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato akizungumza kuhusu kuwepo kwa ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Japan katika suala la Maendeleo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Jijini Dar es Salaam.

Wajumbe walioambatana na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato wakifuatiia kwa makini majadiliano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na mgeni wake ambaye ni Makamu wa Rais wa JICA Bw. Hiroshi Kato, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisisitiza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Hiroshi Kato (hayupo pichani) katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Elijah Mwandumbya akizungumzia mabadiliko ya Sheria ya Kodi yaliyofanywa hivi karibuni ambayo yanalenga kutoa misamaha ya kodi yenye tija kwa umma wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Kamishina Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi akielezea kuhusu masuala ya kodi katika maendeleo ya Taifa katika mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato walipokutana kwa mazungumzo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan –JICA nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase, alioambatana na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Bw. Hiroshi Kato (katikati) walipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

No comments: