Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kushoto) na Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Farmster ya Israel, Adam Abramson wakitia sahihi mkataba wa makubaliano ambapo Farmster itatoa huduma za upatikanaji wa masoko ya mazao na bidhaa za wakulima wanachama wa Mkikita kwa njia ya mtandao wa simu. Hafla hiyo ilifanyika viwanja vya Camp of Good Hope, Goba jijini Dar es Salaam.
Abramson ambaye ni mwasisi wa Farmster aliwaelezea waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo jinsi jinsi ya kujiunga na mtandao huo kwa kutumia simu za smart na za kawaida yaani 'vitochi' ambapo mkulima huingiza namba ya simu 0623 753016 kwa kutuma neno Jambo.
Mkulima atapaswa kutaja jina lake, eneo analoishi yaani shamba lilipo, analima zao gani, heka ngapi na anatarajia kuvuna lini na kwa kiasi gani ambapo huunganishwa moja kwa moja kwa mteja atakayejadiliana bei ya kuuzia.
Wakala Mkuu kati ya Mkulima na Mnunuzi utakuwa ni Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA), kitendo ambacho kitasaidia sana kuuvunja mtandao wa madadali wanaosumbua na kuwaibia wakulima.
Wakulima waliohudhuria hafla hiyo walionekana kufurahishwa na ujio wa teknolojia hiyo mpya na ya kisasa itakayowarahisishia wakulima kupata masoko mazao yakiwa shambani.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kushoto) akibadilishana hati za makubalino baada ya kutiliana sahihi mkataba na Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Farmster ya Israel, Adam Abramson ambapo Farmster itatoa huduma za upatikanaji wa masoko ya mazao na bidhaa za wakulima wanachama wa Mkikita kwa njia ya mtandao wa simu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Dk. Kissui S. Kissui (kushoto), akimpongeza Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Farmster ya Israel, Adam Abramson kutiliana sahihi mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange (katikati) ambapo Farmster itatoa huduma za upatikanaji wa masoko ya mazao na bidhaa za wakulima wanachama wa Mkikita kwa njia ya mtandao wa simu.
Abramson akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo
Akionesha namba ya kujiunga na mtandao huo
Wanachama wa Mkikita wakisikiliza wakati mtalaamu huyo akiwaelezea faida mbalimbali atakazopata mkulima kwa kutumia mtandao huo
Abramson akionesha eneo alipo mmoja wa wakulima aliyejiunga na mtandao huo
Mkulima akipata maelezo kutoka kwa Abramson
Wakulima wakiwa makini kumsikiliza mtalaam huyo
Dk. Kissui ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita akiwatambulisha wakurugenzi wa bodi ya Mkikita.
Wakulima wanachama wa Mkikita wakiwa katika hafla hiyo
Maofisa wa Mkikita wakiwa katika tukio hilo
Dk Kissui akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo
No comments:
Post a Comment