ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 21, 2017

FAINALI YA MASHINDANO YA MISS TANZANIA YAPIGWA KALENDA

Kampuni ya Lino International Agency Limited, waandaji wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania tunapenda kuwajulisha wapenzi, mashabiki na wadau wa tasnia ya urembo kwamba hakutakuwa na Fainali za Taifa za shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2017.
Sababu kubwa za kuahirishwa kwa Fainali hizi ni ukosefu wa Wadhamini ambao kwa njia moja au nyingine huwezesha kufanyika kwa mashindano hayo kwa kulipa gharama mbalimbali ikiwemo zawadi za washiriki n.k.
Aidha kuchelewa kupata kibali cha kuanza mchakato wa Miss Tanzania 2017 pia kumechangia kukosa Wadhamini kutokana na muda kuwa mfupi. Kibali cha kuendesha mashindano ya Miss Tanzania 2017 kimetolewa na Basata mwezi Septemba 2017.
Washindi wa Mikoa na Kanda ambao tayari wameshinda katika sehemu mbalimbali ambao wamefanya mashindano yao kwa mwaka 2017 watashiriki Fainali za Taifa kwa mwaka ujao wa 2018 katika tarehe na mwezi ambao tutawajulisha hapo baadae.
Baadhi ya Mikoa na Kanda mbalimbali ambao hawakuweza kufanya mashindano yao kwa mwaka 2017 kutokana na changamoto za udhamini, tunawapa muda wa kujipanga upya hadi mwezi Mei 2018 wawe wamefanya mashindano yao ili kutoa nafasi kwa Fainali za Taifa kufanyika.
Aidha tunapenda kuchukua fursa hii kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini mashindano ya Miss Tanzania 2018  ili kutoa fursa kwa wasichana washiriki ambao ndio walengwa wa mashindano haya.

Kamati ya Miss Tanzania inawataka Mawakala wote wa Miss Tanzania kufuata Kanuni, Sheria na Taratibu za Mashindano ikiwa ni pamoja na kusajiliwa na kulipa ada husika Baraza la Sanaa la Taifa, kuandaa shindano lenye hadhi na  kutoa zawadi kwa wakati.

Mawakala pia wanatakiwa kuwa na ofisi na mawasiliano yanayoeleweka.
Wakala ambaye hatotimiza masharti hayo, shindano lake halitotambuliwa na hivyo kuwanyima fursa washiriki wa mashindano haya.


Uongozi wa Kampuni ya Lino International Agency Limited tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa ushirikiano wao ambao wamekuwa wakitupatia kila mara tunapohitaji kufanya hivyo.



HIDAN .O. RICCO.

AFISA HABARI.
0673 019112

No comments: