ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 1, 2017

KAIMU BALOZI INMI PATTERSON AFANYA ZIARA MKOANI MWANZA


Ubalozi wa Marekani
Dar es Salaam
TANZANIA
29 NOVEMBA, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dar es Salaam, TANZANIA. Kutoka tarehe 26 had 28 Novemba, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson alifanya ziara mkoani Mwanza kwa lengo la kukuza uelewa wa wananchi kuhusu jitihada zinazofanywa na Marekani katika kujenga uwezo wa Watanzania katika kujenga jamii zenye afya, kukuza uchumi wa jamii na mkoa na kusaidia elimu.

“Serikali ya Marekani ina fahari kufanya kazi na Watanzania, ikiunga mkono na kusaidia jitihada za wananchi wenyewe za kujenga Tanzania yenye Amani, ustawi, usalama na afya,”alisema Kaimu Balozi Patterson akiwa ziarani katika Shule ya Wauguzi ya Askofu Anthony Mayalla iliyopo katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambako wauguzi wa Kimarekani wanafanya kazi pamoja na kuwafundisha wenzao wa Kitanzania mbinu za kuwahudumia watoto wachanga na akina mama waliojifungua kama sehemu ya sehemu ya mpango wa Ubia wa Kutoa Huduma za Afya Duniani (Global Health Service Partnership)
“Uhusiano wetu mkubwa unaakisiwa na ushirikiano wa kina baina ya nchi zetu mbili, na ninaimani kuwa tutaendelea kuimarisha uhusiano wetu huu wa kihistoria tunapoendelea kusaidiana.”

Ukiwa mkoa muhimu katika ushirikiano kati ya Serikali ya Marekani na Tanzania, Mwanza ni mwenyeji wa miradi kadhaa ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani ikiwa ni pamoja na Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps, Programu mbalimbali zinazoendeshwa chini ya Mpango wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI kwa kupitia Taasisi ya Kimarekani ya Udhibiti wa Maradhi (CDC) na jitihada za maendeleo zinazoongozwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID). Ushirikiano wa maendeleo na wabia wa Kitanzania ni sehemu ya uwekezaji mkubwa na ushirikiano kati ya serikali ya Marekani na watu wa Tanzania.

Picha kuhusu ziara hizo kwa matumizi ya vyombo vya habari, kwa hisani ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam, zinaweza kupatikana mtandaoni kwa kupitia anuani: https://flic.kr/s/aHsm6E15H1

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au kwa barua pepe: DPO@state.gov.

No comments: