Advertisements

Saturday, December 30, 2017

Ndanda FC yamsajili Mrisho Ngasa kuiua Simba

By Haika Kimaro, Mwanaspoti

Mtwara. Kuelekea katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara kesho Jumamosi dhidi ya Simba SC, Ndanda FC ya mkoani Mtwara imetangaza usajili wa wachezaji watatu waliongezwa kikosini katika dirisha dogo.

Katika tarifa ambao imetolewa na Ofisa Habari wa Ndanda FC, Idrissa Bandari amewataja wachezaji hao ni kiungo Mrisho Ngasa aliyemalizana na Mbeya City, mshambuliaji Ame Ali aliyekuwa Kagera na kiungo Salum Telela ambao wote wamesaini mkataba wa miezi Sita

“Tumefanya maboresho ya kuongeza watu wachache katika kikosi ambao tumewasainisha mkataba wa miezi sita tumeona wanaweza kuja kuhudumia katika kikosi chetu,” amesema Bandali.

No comments: