Marekani imefeli kuulazimisha ulimwengu kukubaliana na azimio lake lililokinyume na sheria, wakati mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipopitisha kwa idadi kubwa ya wanachama wake,kupinga azimio la Trump linaloitambua Jerusalem kama Mji Mkuu wa Israeli.
Pamoja na vitisho vya Marekani kwa nchi za dunia kuwa itainyima misaada ya kifedha, kupitia Mwakilishi wake katika Umoja huo wa Mataifa kwamba “Aidha fedha au kulipitisha azimio”, Marekani na Israeli pamoja na nguvu zao hazikuweza isipokuwa kuzikinaisha nchi 7 tu, katika kupigia kura ya hapana azimio hilo zikiwemo zenyewe.
Nchi 128 zimelipigia kura ya ndio azimio hilo,ambazo ni sawa na watu bilioni 7 walio ulimwenguni, sawa na asilimia zaidi ya 90% ya wakazi wote, huku azimio hilo likiwa linalazimisha kuwa kwake, kwa kupata zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wakamati kuu ya mkutano mkuu, likiwa na uzito sawa na maazimio ya Baraza la Usalama.
Tanzania vilevile imepigia kura ya ndio azimio hilo ikiwa pamoja na nchi nyingi duniani, zikiwemo China, India, Urusi, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na idadi kubwa ya nchi za Umoja wa Ulaya, nchi zote za kiislamu na kiarabu pia nchi nyingi za Amerika ya Kusini.
Kilichoshangaza zaidi ni kuona dola ya Vatikani imepinga azimio la Trump, dola ambayo yenyewe inawakilisha ulimwengu wa kikristo, huku yakiwa makubaliano ya kiislamu, kikristo na kibinaadamu yote yanapinga azimio la Trump lisilo la kisheria na si la kiuadilifu, ambalo pia linakwenda kinyume na kanuni na sheria zote za kimataifa.
No comments:
Post a Comment