ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 5, 2018

BALOZI MTEULE WA UFARANSA AWASILISHA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier ambaye alifika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje leo kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frédéric Clavier.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frédéric Clavier baada ya Mhe. Balozi kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho. Wawili hao pamoja na mambo mengine walizungumzia masuala ya uwekezaji ambapo Ufaransa inahitaji kuongeza uwekezaji wa makampuni yake hapa nchini ili kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Ujumbe wa Wizara ulioshiriki mazungumzo hayo. Kutoka kulia ni Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga; Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. Jacob Msekwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Balozi Mteule wa Ufaransa wakiendelea na mazungumzo yao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiteta jambo na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier mara baada ya wawili hao kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi zao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier wa pili kutoka kushoto. Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) na Naibu Balozi wa Ufaransa, Bw. Alexandre Peaudeau.

No comments: