Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Mpina (mwenye kofia) akipata maelezo ya hali ya sekta ya mifugo na Uvuvi kutoka
kwa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Denis Mwila (mwenye
suti
nyeusi) alipotembelea kituo cha mpakani cha
Mutukula leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Mpina (mwenye kofia) akipokea maelezo ya
changamoto za ukaguzi mazao ya mifugo na Uvuvi
kutoka kwa Afisa Uhamiaji Konstabo, Rahabu Joel alipotembelea kituo cha
mpakani cha Mutukula leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Mpina (mwenye kofia) akiangalia mabondo ya samaki aina ya Sangara yaliyokamatwa
katika kituo cha mpaka cha Mutukula
mkoani Kagera. Kulia ni kaimu Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo
ya Uvuvi Mwanaidi Mlolwa
katikati Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya
Missenyi Limbe Maurice. Kilo120
zilikamatwa katika kituo hicho.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Mpina akifungua mlango wa gari lililokamatwa na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya
ya Ngara likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina
ya Sato zenye thamani ya shillingi
20,850,000/= kwenye
mpaka wa Mlusagamba wilayani
Ngara tarehe 03/12/2017
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina ya
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kuhakikisha
inafufua mara moja mnada wa Mlusagamba ifikapo mwezi Februari mwaka huu ili
kudhibiti zaidi ya milioni mia moja zinazopotea kwa wafanyabiashara wanaokwepa
kulipa kodi ya Serikali ya kusafirisha mifugo nje ya nchi kwa kupita njia za
panya.
Waziri Mpina aliyasema haya leo alipokutana na uongozi wa
Halmashauri hiyo pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara
katika kituo cha mpaka cha Rusumo baina ya Tanzania na Rwanda kukagua shughuli
mbalimbali za sekta za Mifugo na Uvuvi
baada ya kutokea katika kituo cha Mutukula mkoani Kagera ambapo pia
alifanya ukaguzi kama huo na kukamata kilo 120 za mabondo ya samaki aina ya
Sangara yaliyokuwa yakitokea nchi jirani ya Uganda bila kufuata
utaratibu.
“Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya sekta ya mifugo na uvuvi
naelekeza kwamba ifikapo Februari mwaka huu nataka miundo mbinu yote iwe
imeboreshwa na mnada wa Mlusagambo uwe unafanya kazi katika kiwango cha mnada
wa upili na mimi mwenyewe nitahakikisha ninakuja kuuzindua”lisisitiza
Mpina
Waziri Mpina alisema kutokuwepo kwa Mnada wa Mlusagambo
kunaipotezea Serikali mapato makubwa ambapo mifugo mingi imekuwa ikiuzwa katika
nchi jirani na Serikali kuambulia kiasi kidogo cha fedha kutokana na
wafanyabiashara kupita njia za panja na kufanikiwa kukwepa kulipa kodi
malimbali za Serikali.
Alisema taarifa inaonyesha kuna idadi kubwa ya
Ng’ombe wanaopita njia za panya ambao
hawatozwi ushuru wa kushafirishwa
jambo ambalo amelilalamikia kuwa ni
hujuma
na kuendekeza rushwa baina ya
watendaji wa Serikali.
Aidha amesema Wizara inakusudia kuomba Serikali kupandisha
ushuru wa kusafirisha mifugo (movement permit) kufikia shilingi 50,000/= badala
ya shilingi 20,000/= ya sasa kwa kuwa hailingani na
hali halisi ya soko na gharama za utunzaji
wa mifugo hiyo.
“Tutahakikisha tunaiomba serikali ibadili ushuru huu kwa kuwa
mfugaji anatumia gharama kubwa za kumfuga na kumnenepesha mfugo kwa zaidi ya
miaka mitano halafu anakuja kupata shilingi 20000 tu ni jambo lisilokubalika”
alisisitiza Mpina
Aliongeza kwamba baada ya kukamilika kwa mnada huo Serikali
itaweka vizuizi katika njia zote za panya ambapo pia alisisitiza
watendaji wa Serikali
na wananchi kwa ujumla kuwa
waadilifu na kuwa walinzi badala
ya kutegemea viongozi wa kitaifa wa Serikali
kulinda
utoroshaji wa raslimali za taifa ikiwa ni pamoja na mifugo,
samaki na mazao mbalimbali yatokanayo na sekta
hizo.
Aidha alisema katika njia zote za panya inashangaza kuona
kuna wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji, kata, vyombo vyote vya serikali
vya ulinzi na usalama pia kuna Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya lakini utoroshaji
unaendelea bila wahalifu hao kukamatwa, ambapo aliwataka watendaji wote kuwa
waaminifu na kumwagiza Mkuu wa Wilaya kuwachukulia hatua za mara moja watendaji
watakaobainika kujihusisha na vitendo viovu ikiwa ni pamoja na
rushwa.
Akitolea mfano wa jinsi alivyokamata kilo 65,600 za samaki
wachanga aina ya Sangara waliokaushwa kwa chumvi wenye thamani ya shilingi
milioni mia tatu katika Kisiwa cha Lubili wilayani Muleba kwenye Mkoa wa Kagera
baada ya wamiliki wa samaki hao kukimbia hivi karibuni,
alisema zoezi hilo lilifanikiwa baada ya yeye
kupata
taarifa kutoka kwa raia mwema ambapo
aliagiza mamlaka za Wilaya ya Muleba kufuatilia kwa karibu hatimaye
kuwakuta samaki hao wakiwa wameanikwa
chini katika kisiwa hicho.
“Naomba kusema raia mwema huyo alitoa taarifa siyo kwa sababu
alilipwa fedha bali alikuwa na uchungu
na uzalendo wa dhati kwa taifa lake baada ya kuona kwamba
raslimali ya taifa inatoweka” alihoji Waziri
Mpina
Aidha, Waziri Mpina alisema Wizara inapambana kuhakikisha
kwamba kunakuwa na kodi ya mifugo ambapo kila mfugo utatakiwa kulipiwa kodi
tofauti na mfumo wa sasa ambapo hakuna kodi ya moja kwa moja inayotozwa kwa
mifugo.
Alisema uanzishwaji wa
kodi ya mifugo utasaidia kuleta mapinduzi makubwa ya mifugo katika kipindi
kifupi kijacho kwa kuwa fedha
itakayokusanywa itatumika katika kununua madawa ya ruzuku kwa mifugo, chanjo,
kuboresha malisho na miundombinu mbalimbali
ya mifugo ikiwa ni pamoja na majosho na malambo ya
kunyweshea maji mifugo
hiyo.
Alisema taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa asilimia 30 ya
mifugo yote nchini inateketea nchini wakati wa jua kali kipindi cha kiangazi
kwa sababu ya kukosa maji na malisho bora jambo ambalo
ni hasara kubwa kwa taifa.
Mbunge wa jimbo la Ngara, mheshimiwa,Alex Raphael Gashaza
alipendekeza
wafugaji kutambuliwa kwa kulipa kodi ya mifugo na kuanzisha vitalu maalumu vya
ranchi za mifugo ili kuthibiti magonjwa na kuinua ubora wa
mifugo.
Alisema utaratibu huo pia utapunguza migogoro mingi
inayojitokeza sasa baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi ambapo
ambapo pia ameipongeza Serikali kwa juhudi inazofanya katika zoezi
linaloendelea la kupiga chapa mifugo.
Akitoa ufafanuzi Waziri Mpina alisema Serikali inaruhusu
uanzishwaji wa ranchi ndiyo maana suala
hilo limezingatiwa katika sheria mbali mbali za tasnia ya mifugo ikiwa ni
pamoja na Sheria ya Utambuzi, Usajili na
Ufuatiliaji Mifugo Namba 12 ya Mwaka
2010, Sheria ya Nyanda za Malisho na Vyakula vya Mifugo Namba 13 ya Mwaka 2010,
na Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo namba 4 ya Mwaka
2012.
Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luteni Kanali
Michael Mtenjele alimweleza Waziri kuwa
katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba mwaka 2017 jumla ya kilo 903,018
za mazao ya uvuvi kutoka katika maeneo ya Mwanza,Mganza,Kagera, Kigoma na Dar
es Salaam yenye thamani ya shilingi
bilioni mbili yalikaguliwa na kuhakikiwa na kuruhusiwa kusafirishwa
kupitia kituo cha mpakani cha Rusumo.
Aidha alisema kituo cha Rusumo katika kipindi hicho kimekusanya
shilingi 7,058,300 kama mrahaba kwa mazao ya uvuvi yanayokwenda nje ya
nchi.
Akiwa katika ziara hiyo Waziri Mpina alipata fursa ya kuliona
na kukagua gari lenye namba za uasajili
T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter lililokamatwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama
ya Wilaya ya Ngara likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo
530 wa aina ya Sato zenye thamani ya
shillingi 20,850,000/= kwenye mpaka wa
Mlusagamba wilayani Ngara tarehe 03/12/2017 saa tatu asubuhi ambapo
aliwaelekeza watendaji kuhakikisha taratibu zote za kisheria zinafuatwa ili
kuweza kulitaifisha gari hilo kulingana
na Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka
2003 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2012 na
2015.
Katika tukio hilo Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa
Uvuvi
wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana
Ayoub Ngoma na dereva wa
gari hilo Ayoub Sanga walishikiliwa na polisi
ambapo Ngoma
alisimamishwa kazi mara moja kupisha uchunguzi.
Aidha Mshauri wa Uvuvi wa Mkuu wa Mkoa, Efrazi Mkama
na maafisa Uvuvi wa Halmashauri ya Muleba
Wilfred Tibendelana na Maengo Nchimani na Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Bukoba vijijini Renus Ruhuzi wanaendelea kuripoti katika kituo cha polisi
Bukoba kwa mahojiano ya kisheria juu ya utoroshwaji wa samaki
hao.
No comments:
Post a Comment