TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI
KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MFUKO WA
HIFADHI YA JAMII KWA WATUMISHI WA UMMA, 2017(THE PUBLIC
SERVICE SOCIAL SECURITY FUND ACT, 2017), KUHUSIANA NA
MASUALA YA KODI, MAFAO YA MAJAJI NA MAFAO
YATAKAYOTOLEWA
KWA WATEGEMEZI
Kumekuwa na tafsiri potofu
kuhusu Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi
wa Umma (The Public Service
Social Security Fund Act, 2017), inayotolewa aidha kwa bahati mbaya au kwa
lengo la kupotosha maudhui ya Muswada huo kuwa unakusudia kutoza kodi mafao ya Wastaafu, kubagua
Wajane na kuathiri mafao
ya Majaji.
Tunapenda kuutaarifu Umma na Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi
ya Jamii kwa ujumla
kwamba tafsiri hiyo siyo sahihi na ni upotoshaji mkubwa na kwa misingi hiyo tunapenda
kutoa taarifa na ufafanuzi kama ifuatavyo:
1.0. Serikali
haijawahi na wala haikusudii kutoza kodi Mafao ya
Wanachama na wala si malengo ya kifungu
cha 56 cha Muswada
huu. Ni vema ifahamike kwamba
hata katika Sheria
za sasa za Mifuko
ya Pensheni na Sheria za Kodi, mafao ya wanachama
hayatozwi kodi, rejea
kifungu cha 47(3)
cha Sheria ya Mfuko PSPF, kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Mfuko wa GEPF, kifungu cha
90(2) cha Sheria
ya Mfuko wa NSSF na kifungu cha 54 cha Sheria ya Mfuko wa PPF. Aidha,
masharti na maudhui
ya kifungu cha 56 cha Muswada
yanafanana kabisa na masharti ya vifungu
tajwa hapo juu vikisomwa pamoja na sheria za kodi ambazo ndiyo misingi wa misamaha yote ya
kodi nchini.
2.0. Masharti kuhusu
mafao ya Majaji yamechukuliwa kutoka kwenye
Sheria ya Mfuko wa PSPF ambako ni vifungu vya 21 na 22 vya Sheria Hiyo. Hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika kwenye maudhui ya vifungu hivyo zaidi ya kuboreshwa kwa kutenganisha masharti ya Pensheni na stahili nyingine. Hivyo taarifa
zinazotolewa kwenye vyombo
vya habari kuhusu mafao ya Majaji
ni upotoshaji wa makusudi unaolenga kujenga taswira potofu mbele ya macho ya Jamii.
3.0. Eneo la mafao ya Wajane na warithi
katika Muswada ni moja ya maeneo
ambayo yameboreshwa kwa kiasi kikubwa
ikilinganishwa na masharti yalivyo kwenye Sheria za sasa. Muswada umebainisha kwa uwazi stahili za Wajane na Warithi pale mwanachama au mstaafu anapofariki.
Tunawashauri na kuwaasa wananchi na Taasisi nyingine
kuepuka kutoa maoni ambayo
yanalenga kupotosha nia njema ya Serikali katika Muswada huu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya
Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
Dar es Salaam
22/1/2018
No comments:
Post a Comment